Tetesi za soka Ulaya Jumatano 21.03.2018

Winga wa Manchester United Anthony Martial
Image caption Winga wa Manchester United Anthony Martial

Ajenti wa mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22, hajatoa hakikisho lolote kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kusalia katika klabu hiyo. (Il Bianconero, via Independent)

Tottenham imejiandaa kumpoteza beki wa ubelgiji Toby Alderweireld, 29, mwisho wa msimu huu lakini watahitaji kulipwa dau la Yuro 50m (£44m). (HLN - in Dutch)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Liverpool imesema kuwa haitamuuza mshambuliaji wake Mohamed Salah

Liverpool imesema kuwa haitamuuza mshambuliaji wake Mohamed Salah, 25, mwisho wa msimu huu na kwamba mchezaji huyo wa Misri hana kandarasi itakayomruhusu kuondoka katika klabu hiyo wakati wowote. (ESPN)

Liverpool bado haijwasiliana na kipa wa Roma Alisson, 25, lakini raia huyo wa Brazil hayuko tayari kutia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Itali. (Sun)

Image caption Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'golo Kante

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 26, amepinga uvumi kwamba anatakakujiunga na PSG kwa kusema kwamba anahisi kuwa nyumbani Stamford Bridge.(Express)

Mchezaji anayelengwa na klabu ya Manchester United Milan Skriniar, 23, anasema kuwa anafurahia kusalia Inter Milan .Ria huyo wa Slovakia pia ameivutia Barcelona . The Slovakian also interests Barcelona. (star)

Image caption Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anasema kuwa kujiamini ndio ufunguo wa ufanisi

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anasema kuwa kujiamini ndio ufunguo wa ufanisi .Mchezaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33 amefunga mbao 21 katika mechi 13 tangu kuanza kwa msimu wa 2018.2018. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure hakushiriki katika mazoezi ya kwanza na timu ya taifa ya Ivory Coast siku ya Jumanne . (Fifciv.com)

Image caption Yaya Toure

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amewapatia wachezaji wake ambao hawajiungi na timu zao za kimataifa likizo ya wiki moja huku akiwapeleka ,wasaidizi wake wa ukufunzi Tenerife. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaipata mashakani na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kujihusisha na kampuni nyengine ya kucheza kamari.. (Mirror)

Image caption Zlatan Ibrahimovic

Kampuni ya Vodafone nchini Misri itapeana masalio ya kupiga simu kwa wateja wake wote kila baada ya mshambuliaji wa Liverpool Mohamed salah kufunga bao. (mirror)

Chelsea inaongoza katika kumnyatia beki wa Ujingereza na Man United Luke Shaw, ambaye alikuwa shabiki mkubwa Chelsea akiwa utotoni mwake , iwapo ataamua kuondoka manchester United mwisho wa msimu huu. (Mail)

Image caption Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha

Maafisa wakuu katika klabu ya Manchester United wanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu tabia ya Mourinho dhidi ya Shaw na hatua hiyo huenda ikaathiri thamnia ya uhamisho ya mchezaji huyo (Telegraph)

Tottenham iko tayari kurudi Crystal Palace na dau la £40m kumsajili winga Wilfried Zaha, 25, lakini Crystal Palace inaamini kwamba mchezaji huyo ana thamnia ya juu zaidi.. (Mail)

Mada zinazohusiana