Luke Shaw: Ashley Young atofautiana na Jose Mourinho

Luke Shaw Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luke Shaw meichezea Manchester United mara 15 msimu huu

Beki wa Manchester United Luke Shaw anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani kulingana na mchezaji mwenza Ashley Young.

Shaw, 22, alikosolewa hadharani na mkufunzi Jose Mourinho baada ya kutolewa nje wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi ambapo United iliibuka washindi kwa 2-0.

Young, 32, amekuwa chaguo la Mourinho katika safu ya beki wa kulia katika kipindi kirefu cha msimu na kama Shaw alitajwa katika kikosi cha Uingereza kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Uholanzi na Itali.

''Ni mchezaji mzuri sana'' , alisema Young.

Shaw ambaye alijunga na Southampton kwa dau la £27m 2014 ana kandarasi na United hadi mwezi Juni 2019 lakini huenda akaondoka United mwisho wa msimu huu.

Mourinho amemkosoa Shaw mara kwa mara hapo awali na kuhoji tabia ya beki huyo katika mazoezi mbali na kujitolea kwake katika klabu hiyo Aprili iliokwisha.

Shaw ambaye ameichezea Uingereza mara saba hajacheza tena katika timu hiyo tangu Machi 2017.

''Nataka kuona Luke anacheza vyema na kufanikiwa'', alisema Young. ''lazima ajitolee na kujiimarisha. Nahisi anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Young anasema kuwa wachezaji wa United wanajua ni wakati gani wanafaa kujitolea zaidi chini ya Mourinho

Mourinho amekuwa akikosolewa huku aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal BBC Radio 5 live akisema kwamba hawezi kukubali kucheza chini ya ukufunzi wa Mourinho.

United ni ya pili katika jedwali la ligi na wako katika nusu fainali kombe la FA lakini walibanduliwa katika kombe la vilabu bingwa Ulaya wiki iliopita na aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Chris Sutton anaamini kwamba Mourinho amepitwa na wakati.

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 55 anaonekana kuungwa mkono na wachezaji wake huku Young akisema kuwa wachezaji wenzake wanajua msimamo wao.

''Mkufunzi huyu amefanikiwa katika kila klabu ambayo amefunza'', alisema.

''Sidhani kama angepata ufanisi alioupata iwapo hajui kushirikiana na wachezaji. Tunajua kama wachezaji tunakwenda katika uwanja wa mazoezi na kujitahidi, na iwapo unaweza , anacheka na kutoa mzaha, hivyobasi ana pande zote mbili na hiyo ni tabia nzuri kwa mkufunzi''.

Mada zinazohusiana

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea