Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 29.03.2018: Manchester City kuzungumza na Sterling, Chelsea wanamtaka kinda wa miaka 15

Raheem Sterling Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester City wanatarajia kuanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya na winga Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kumalizika kwa msimu . Mchezaji huyo wa kikataifa wa England ana miaka miwili iliyosalia kwenye mkataba wake. (ESPN)

Tottenham wanamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Lisbon Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 23, lakini watatakiwa kulipa kitita cha Euro milioni 87 kusaini mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno . (Abola - kwa Kireno)

Image caption Mlinzi wa Arsenal mJerumani Shkodran Mustafi anasema timu yake ilikuwa na kikao cha kuijadili matokeo mabaya ya timu yao baada ya kufungwa mfulurizo na Man City

Arsenal imefanya mazungumzo juu ya kuhamia kwa mlinzi wa Freiburg Caglar Soyuncu, mwenye umri wa miaka 21. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki amethamanishwa kwa kiwango cha Euro milioni 30 na kilabu cha Bundesliga . (Mail)

Mlinzi wa Arsenal Mjerumani Shkodran Mustafi, mwenye umri wa miaka 25, anasema the Gunners walikuwa na kikao cha timu yao baada ya kushindwa mfululizo na Manchester City kwa lengo la kubadili matokeo yao mabaya . (London Evening Standard)

Chelsea wanakaribia kusaini mkataba na kijana wa Uholanzi Jayden Braaf, mwenye umri wa miaka 15, kutoka timu ya PSV Eindhoven. Manchester City, Manchester United, West Ham na Bayern Munich wote wameelezea nia yao ya kusaini mkataba na mshambuliaji huyo. (Mail)

Everton wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 26, ikiwa ataondoka kwenye kilabu hicho katika msimu huu wa majira ya joto . Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England unakwisha msimu huu wa majira ya joto. (Star)

Image caption Everton wana mzozo wa mkataba na meneja wa zamani wa timu hiyo Ronald Koeman (pichani) kuhusu malipo

Everton wana mzozo wa mkataba na meneja wa zamani wa timu hiyo Ronald Koeman, ambaye kwa sasa ni meneja wa timu ya Uholanzi Netherlands, baada ya kubainika kuwa kilabu hicho kinalipa 90% ya malipo aliyolipwa Muholanzi huyo. (Liverpool Echo)

Watford huenda wakamuuza kwa kiwango cha Euro milioni 40 mchezaji wa kiungo cha kati Abdoulaye Doucoure, mwenye umri wa miaka 25, katika msimu huu wa majira ya joto, huku Liverpool, Tottenham na Arsenal wote wanammezea mate mFaransa huyo. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mourinho amefanikiwa kumshawishi Winga wa Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, kujiunga na Manchester United

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke Ibrahim Afellay, mwenye umri wa miaka 31, ameambiwa awe mbali na klabu hiyo na Paul Lambert, ambaye hapendezwi na tabia ya Mholanzi huyo na kiwango chake katika mazoezi. (Telegraph)

Winga wa Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, ameshawishiwa na meneja wa Manchester United Jose Mourinho kujiunga na klabu hicho ya Ligi ya Premia mwisho wa msimu. (Marca)

Wakati huo huo, Bale ameambiwa na kocha wa Wales Ryan Giggs aendeshe kiti maalum ili kujiepusha na majeraha. (Times)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa Italia Carlo Ancelotti amekataa kazi ya soka ya taifa lake na badala yake anajiandaa kwenda Primia Ligi

Striker Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 36, aliondoka Manchester United baada ya kushindwa kuendelea katika ligi ya klabu bingwa Ulaya, kulingana na daktari aliyemfanyia upasuaji ya goti la mchezaji huyo wa Sweden. Amejiunga na LA Galaxy. (South China Morning Post)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Chukwunonso Madueke, mwenye umri wa miaka 16, baada ya kukataa kusaini mkataba mpya na kilabu hicho cha kaskazini mwa London. (Mail)

Meneja wa Italia Carlo Ancelotti amekataa kuchukua kazi ya kuiongoza timu ya taifa hilo kwani anasubiri kurejea katika Ligi ya Premia ya Ulaya, huku chaguo lake likiwa ni klabu za Chelsea na Arsenal (ItaSportPress - kwa Kitaliano)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nahodha wa Aston Villa John Terry mwenye umri wa miaka 37 ameashiria kuwa ataendelea kubakia kwenye klabu hiyo, licha ya kwamba alitarajiwa kustaafu

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Claudio Marchisio, mwenye umri wa miaka 32, anaweza kuondoka katika kilabu hicho kujiunga na MLS ya New York City. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia katika Turin unamalizika msimu huu wa majira ya baridi. (Tutto Mercato Web - in Italian)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Bournemouth Lewis Cook, mwenye umri wa miaka 21, alimfanya babu yake tajiri wa Euro 17,000 alipochezea kwa mara ya kwanza England dhidi ya Italia siku ya Jumanne. Trevor Burlingham aliweka dau la Euro 500 mnamo mwaka 2014 juu ya ushindi wake kabla hajatimiza umri wa miaka 26. (Telegraph)

Mkurugenzi wa soka wa timu ya Aston Villa Steve Round anasema nahodha John Terry ameashiria kuwa ataendelea kuwa na kilabu hicho. Mlizi huyo wa zamani wa England, mwenye umri wa miaka 37, amekuwa akitarajiwa kustaafu na kurejea katika kilabu cha Chelsea kama kocha. (Birmingham Mail)

Mada zinazohusiana