Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 01.04.2018

Alvaro Morata
Maelezo ya picha,

Alvaro Morata

Real Madrid itajaribu kumrejesha mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kwenda Bernabeu msimu huu kufuatia mchezaji huyo wa miaka 25 kuhamia Chelsea Julai iliyopita kwa rekodi ya pauni milioni 60. (Express)

Manchester United itamchukua mshambulizi mfaransa Anthony Martial, 22, ili kumununua mchezaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28, msimu huu. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Antoine Griezmann

Mshambulizi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amekataa kuhamia Old Trafford na badala yake kuamua kuhamia Barcelona. Mchezaji huyo wa miaka 27 anataka kusalia La Liga kwa pauni milioni 88 akiijiunga na Barcelona. (Sun)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekiri kuwa hana uhakika kuwa atakuwa Stamford Bridge msimu ujao. (Mail)

Maelezo ya picha,

Antonio Conte

Chelsea wanamlenga meneja wa Argentina Mauricio Pochettino, 46, kuchukua mahala pa meneja wake ikiwa atashindwa kumaliza mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake. (Sun)

Chelsea watatumia pauni milioni 30 kumpata nahodha wa Newcastle na mlinzi wa England Jamaal Lascelles, 24, baada ya kuridhishwa na ujuzi wake. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Pep Guardiol

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amemfananisha beki Kyle Walker, 27, na mchezaji wa Bayern Munich Mjerumani Philipp Lahm, 34. (Manchester Evening News)

Schalke imethibitisha kuwa mchezaji wa kimataifa mjerumani, Max Meyer atandoka klabu hiyo msimu huu huku Arsenal na Liverpool wakimwinda mchezaji huyo.

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Emmanuel Frimpong anasema bado anampenda Arsene Wenger, miaka minne tangu aondoke klabu hiyo. (Telegraph)