Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 03.04.2018

Manchester United goalkeeper David de Gea

Chanzo cha picha, Getty Images

Kipa wa timu ya Manchester United, David de Gea (27) anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka tano inayo na thamani ya paundi £350,000 kila wiki. (Sun)

Timu ya Tottenham wanamatumiani kuwa meneja Mauricio Pochettino na wachezaji sita wakuu watasaini makubaliano mapya katika miezi michache inayokuja (Telegraph)

Toby Alderweireld

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Toby Alderweireld

Timu ya Paris St-Germain wakotayari kumpatia mlinzi Tottenham Toby Alderweireld, 29, mkataba anayoutaka wa paundi milioni 10m-kwa kila msimu kwa miaka mitano wakati Mbelgiji huyo anatarajiwa kuondoka Spurs baada ya mazungumzo kuhusu makubaliano mapya yaliisha. (Mail)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atakuwa na timu dhaifu dhidi ya mechi na Manchester United Jumamosi hii, ambapo kishindo ingewapatia tuzo ya Premier League. (Express)

Derek McInnes

Chanzo cha picha, SNS

Maelezo ya picha,

Derek McInnes amewahi kukataa kuhamia timu za Sunderland na Rangers

Derek McInnes, Craig Shakespeare, Michael Appleton, Dean Smith na Graham Potter wako katika orodha ya kuchaguliwa kuwa meneja wa West Brom manager katika majira ya joto. (Times)

Mmiliki wa timu ya Chelsea Roman Abramovich hajafurahishwa na jambo la klabu kukosa kucheza katika ligi ya Champions lakini anasita kumfuta kazi meneja Antonio Conte,ambaye maebakia na mwaka mmoja katika mkataba wake yenye thamani ya paundi milioni 9.5.(Express)

Chelsea wanakabiliana na uwezekano wa kuwapoteza wachezaji tisa katika timu ya kwanza majira ya joto (Telegraph)

Marcos Alonso

Chanzo cha picha, Empics

Mlinzi wa Uhispania na Chelsea Marcos Alonso, 27, anasema kuhangaika kwa timu yake msimu huu imesababishwa na wao kukosa 'uendelevu' na 'bahati' uliowasaidia awali chukua tuzo ya ligi ya Premiere msimu uliopita. (Star)

Liverpool wanamatumaini ya kumpata Valencia Ferran Torres, ikiwa pia timu ya Chelsea pia wanamtaka kijana huyo wa umri wa miaka 18 (Mail)

Everton itatakiwa kukabiliana na vilabu tatu vya Uhispania kama wakitata kumpata mlinzi Wilfried Kanon kutoka Ivory Coast (Sun)