Manchester city yachapwa 3-0 na Liverpool: Uefa

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi

Michuano ya klabu bingwa barani Ulayani, hatua ya robo fainali inaendelea usiku wa kuamkia leo. Michezo miwili imepigwa ambapo Barcelona wakiwa nyumbani dhidi ya As Roma wamepata ushindi wa mabao 4-1.

Mabao ya Barcelona katika mchezo huo, yamefungwa na wachezaji De Rossi ,Kostas Manolas ambao walijifunga wenyewe.Goli la tatu limefungwa na Gelard Pique huku bao la nne likipachikwa na Luis Suarez, bao la kufutia machozi la As Roma likifungwa na Edin Dzeko.

Katika mchezo mwingine Liverpool wao wamewachapa bila huruma vinara wa ligi kuu ya England Manchester city bao 3-0, Magoli ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah, Oxlade Chamberlin pamoja na Sadio Mane.

Robo fainali nyingine ya pili itafanyika tarehe 10 mwezi April kwa michezo miwili,As Roma itacheza dhidi ya Barcelona na Manchester City itachuana na Juventus, na Aprili 11 Bayen Munich itacheza na Sevilla huku Real Madrid ikicheza na Juventus.