Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 06.04.2018

Willian of Chelsea celebrates

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

Willian

Manchester United wanahakika ya kumsajili kiungo kutoka Brazil, Willian kwa paundi milioni 30,wakati kiungo Mhispania Juan Mata anatarajiwa kuondoka Old Trafford (Sun)

Kiungo wa Liverpool, Muuingereza James Milner amesema hata katisha ustaafu wake kutoka mechi za kimataifa. (Times)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Mick McCarthy

West Brom hawana mipango ya kumteua mkuu wa Ipswich, Mick McCarthy kama meneja wao baada ya kuondoka kwa Alan Pardew wiki iliyopita.(Express and Star)

Aliyekuwa mshambulizi wa Liverpool atakuwa mejea wa timu ya Feynoord ya chini ya miaka 19 msimu ujao. (mtandao wa Feynoord)

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Emre Can

Kiungo wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 24, aweza kosa kucheza katika mdimu uliobakia na hata kombe la dunia kwa sababu ya tatizo la mgongo (Mirror)

Qatar itashiriki kama nchi mualikwa katika michuano ya Copa America 2019 (Globo Esporte)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Chris Coleman endured a frustrating afternoon on his return to the Cardiff City Stadium as his Sunderland side lost 4-0

Chris Coleman anasema atabaki kama meneja wa Sunderland hata kama Black Cats wakishushwa na kuwekwa League One. (Mail)

Msahmbulizi wa Watford Richarlison, 20, amehakikishwa nafasi yake katika Vicarage Road hata baada ya kuachwa kwa kushindwa kufunga goli yoyote katika michezo 21.(Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Thomas Tuchel

Aliyekuwa Menejwa wa Dortmund Thomas Tuchel atachukua nafasi ya Unai Emery kama mkuu wa Paris St-Germain kwenye msimu ujao. (ESPN)

Mshambulizi wa Stoke, Saido Berahino, 24, ametolewa kutoka kundi la kwanza kwenye timu baada ya kutokea akiwa amechelewa kwenye mechi ya chini ya miaka 23, siku ya Jumatatu (Telegraph)