Tetesi za soka Ulaya Jumapili 08.04.2018:: Pogba, Martial, Neymar, Guardiola, Salah, Mahrez

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mbrazili Neymar anayechezea Paris St-Germain huenda akabadilishwa na Paul Pogba tetesi zinazotolewa na Jose Mourinho zikawa za kweli

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anataka kubadilisha mchezaji wa safu ya kati Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 25, na mshambuliaji Anthony Martial 22 - wote wachezaji wa kimataifa wa Ufaransa kwa ajili ya kumpata mshambuliaji Neymar Mbrazil mwenye umri wa miaka 26 anayechezea Paris St-Germain . (Daily Star Sunday)

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 07.04.2018

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anatarajiwa kuwa meneja anayelipwa vizuri zaidi duniani kwa kusainbi mkataba wa mwaka wa Euro milioni 20 , na hivyo kuendelea kubakia uwanja wa Etihad hadi 2020. (Sunday Mirror)

Image caption Mourinho amemshutumu Guardiola ama kiongozi wa wakala wa Mino Raiola kwa kusema uongo

Mourinho amemshutumu Guardiola ama kiongozi wa wakala wa Mino Raiola kwa kusema uongo baada ya meneja wa Manchester City kudai alikuwa ameambiwa awachukue wachezaji wa safu ya kati Pogba na Armenia na Henrikh Mkhitaryan mwezi Januari. Mkhitaryan, mweney umri wa miaka 29, alijiunga na joined Arsenal kutoka Manchester United mwezi Januari. (Sunday Telegraph)

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 06.04.2018

Paris St-Germain wanapanga kumchukua winga wa Liverpool Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 25 kutoka Misri. (Le10 Sport - in French)Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amefichua kuwa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, hafurahii kuwa Madrid. (Sunday Mirror)

Leicester wako tayari kumnunua James Maddison Muingereza anayeichezea Norway safu ya kati mwenye umri wa miaka 21 kwa euro milioni 17 ikiwa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 27, ataondoka msimu huu wa majira ya joto. (Sun on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale hafurahii kuwa katika Madrid, amesema Zidane

Azma ya Amanda Staveley ya kuichukua Newcastle imerejea kufuatia mazngumzo muhimu na mmiliki wake Mike Ashley yaliyofanyika kwa wiki kadhaa zilizopota.(Sunday Mirror)

Meneja wa Everton Sam Allardyce amejitokeza kama mtu anayewania kuwa meneja wa West Brom ikiwa atafutwa kazi na Goodison Park club. (Sunday Times - subscription required)

Meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini ndiye mtu anayepigiwa upatu zaidi kuchukua nafasi ya meneja wa timu ya Italia baada ya Giampiero Ventura kufutwa kazi kufuatia Azzurri kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia. (Sunday Times - subscription required)

Image caption Everton wamepanga kumnunua winga wa Burnley -Robbie Brady

Polisi ya Manchester -Greater Manchester Police wataandaa mkakati wa kutoa ulinzi zaidi kwa ajili ya basi ya wachezaji wa Liverpool kwa ajili ya michuano ya robo fainali ya Championi Ligi ya Jumanne ya utakaofanyika kwenye uwanja wa Etihad baada ya badi ya Manchester City kushambuliwa kabla ya mechi katika Anfield. (Mail on Sunday

Everton wamepanga kumnunua winga wa Burnley -Robbie Brady, mwenye umri wa miaka 26 mchezaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Ireland. (Sunday Express)

Real Madrid inamtaka meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane ikiwa watataka kumfuta kazi Mfaransa huyo . (Sun on Sunday)

Image caption Meneja wa Leicester Claude Puel anasema mchezaji wa kati wa Uhispania- Vicente Iborra huenda asicheza tena msimu huu baada ya kupata jeraha mguuni

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri amekaribia kuchukua nafasi ya Mtaliano mwenzake Antonio Conte katika Chelsea msimu ujao, huku upande wa Serie A waki mlenga meneja wa Real Madrid Zidane kama meneja wao mbadala. (Sunday Express)

Mkurugenzi wa timu ya Roma Monchi amekanusha madai kwamba klabu hiyo ilipewa mchezaji wa safu ya mashambulizi mwenye umri wa miaka 27 wa Nice na mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli na wakala wa Mino Raiola. (Corriere dello Sport - in Italian)

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 05.04.2018

Meneja wa Leicester Claude Puel anasema mchezaji wa kati wa Uhispania Vicente Iborra, mwenye umri wa miaka 30, huenda hataweza kucheza katika kipindi kilichosalia cha msimu baada ya kupata jeraha la mguu katika waliposhindwa na Newcastle Jumamosi.(Leicester Mercury)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anasema klabu hiyo inasaka taarifa za soka isiyo ya ligi, kwa matumaini ya kumpata mchezaji wa kama wa Leicester - Jamie Vardy ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya England. (Chronicle)

West Ham wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mchezaji wa Fulham mwenye umri wa miaka 25 anayechezea England safu ya nyuma kulia Ryan Fredericks, ambaye kwa mkataba wake unakwisha mwishoni mwa msimu huu. (Mail on Sunday)

Mada zinazohusiana