Roma yalipa deni la Barca, yatinga nusu fainali

soprts Ulaya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa zamani wa timu ya Manchester City , Edin Dzeko and Aleksandar Kolarov, wakishangilia ushindi juu ya wenzao wa timu ya Roma wakati timu yao ya zamani ikitolewa

Roma imefanya maajabu baada ya kuwabamiza Barcelona 3-0 na hivyo kutinga nusu fainali za mabingwa Ulaya kwa faida ya goli la ugenini.

Barca walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na kuingia uwanjani wakiwa na akiba ya magoli, ambapo kutokana na mechi ya kwanza waliyoipiga Roma bao 4-1, Roma ilikuwa inalazimika kuifunga Barcelona 3-0.

Goli la Edin Dzeko dakika za awali za mchezo (6'), na Penalty ya Daniele de Rossi katika kipindi cha pili dakika ya 58 yamekamilishwa na Goli la Mlinzi Kostas Manolas alilofunga zikiwa zimesalia dakika nane tu mechi kufikia mwisho zimewafanya Barcelona pamoja nakuwa na Lionell Messi ambaye hakufurukuta, kuondokakichwa chini katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Umati uliokuwepo Stadio Olimpico ulilipuka mara baada ya kipyenga cha mwisho pale wachezaji wa akiba wa Roma na benchi lao la ufundi walipoingia katikati ya uwanja kushangilia na wachezaji wao.

Kulikuwa na machozi katika nyuso za mashabiki wasiamini kile walichokishuhudia katika mtanange huo ambao haukutegemewa kuisha ulivyoisha.

Roma imekuwa timu ya tatu katika Champions League kuweza kuyapindua matokeo ya namna hiyo ya goli tatu au zaidi. Timu pekee mbili ambazo awali ziliwahi kufanya hivyo ni Deportivo La Coruna dhidi ya AC Milan mwaka 2004 na Barcelona dhidi ya Paris St-Germain msimu uliopita.