Birmigham mwenyeji michuano ya madola 2022

sport, comonwhealth
Image caption Uwanja wa Birmigham Alexander utakavyoonekana baada ya ukarabati

Jumapili hii mji wa Gold Coast Australia utaukabidhi kijiti cha uenyeji wa michezo ya jumuiya ya madola mji wa Birmingham wa Uingereza.

Birmingham inategemea kuwa mwenyeji wa michuano ya jumuiya ya madola ya mwaka 2022.

Mpango wa paundi milioni 70 kukipanua na kukiboresha Alexander Stadium ya Birmingam umetangazwa.Mpango huo utakiboresha kiwanja hicho chenye umri wa Zaidi ya miaka 40 kutoka kuweza kubeba watu 12,700 mpaka watu 40,000.

Tayari picha ya namna kiwanja hicho kinavyotarajiwa kuonekana imewekwa wazi na iwapo mpango utasalia ulivyo basi nchi nyingi zitaweza kuziona rangi za bendera zao kwani paa la Uwanja huo litakuwa na mifuniko ambayo ina rangi za bendera za nchi kadhaa Duniani.

Image caption Uwanja huu una zaidi ya miaka 40

Upanuzi huu utakifanya pia kiwanja hiki kuwa kikubwa zaidi chenye uwezo wa kutumika kwa michezo mbalimbali ya riadha, ukiacha vile vilivyoko London.