Tetesi za soka Ulaya: Guardiola, Bertrand, Seri, Martial, Drinkwater, Mawson

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola
Image caption Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atasiani mkataba wa mwaka mmoja zaidi na timu hiyo

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atasaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kabla ya kumalizika kwa msimu huu. (Mirror)

Tottenham, Manchester United, Everton na Newcastle wanataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya nyuma kushoto wa Southampton Muingereza Ryan Bertrand mwenye umri wa miaka 28. (Sun)

Image caption Mshambuliaji a Manchester United Anthony Martial anataka hakikisho juu ya mustakabal wake katika timu hiyo

Chelsea na Manchester City wameonyesha ari ya kusiani mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Nice Jean-Michael Seri kutoka Ivory Coast mwenye umri wa miaka 26, ambaye alitangaza kipengele cha euro milioni 40za nyongeza kwenye mkataba wake. (L'Equipe - in French)

Mshambuliaji a Manchester United Anthony Martial mwenye umri wa miaka 22- atataka hakikisho juu ya hali yake ya baadae katika klabu hiyo. Alikuwa amepewa mkataba wa miaka mitano lakini anakataa kuuisaini mpaka atakapohakikishiwa muda zaidi wa kucheza. (Times - subscription required)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Muda wa mchezaji wa Paris St-Germain loanee Jese Rodriguez katika Stoke unaonekana umefikia ukingoni

Mchezaji wa zamani wa safu ya kati wa England Leon Osman anaamini kuwa Martial na mshambuliaji mwenzake wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 20, wanapaswa kuondoka Old Trafford kuanza mwanzo mpya. (BBC Radio 5 live)

R.Madrid yatinga nusu fainali ‘kibabe’

  • United pia wamewatuma wachunguzi wao kumuangalia mchezaji wa Swansea wa safu ya ulinzi Alfie Mawson mwenye umri wa miaka 23 raia wa uingereza. (Sun)

Mchezaji wa Chelsea Danny Drinkwater mwenye umri wa miaka 28 raia wa Uingereza anayecheza safu ya kati ataangalia hali yake ya baadae katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Guardian)

Muda wa mchezaji wa Paris St-Germain loanee Jese Rodriguez katika Stoke unaonekana umefikia ukingoni baada ya Muhispania mwenye umri wa miaka 25- kutokwenda mazoezini Jumatano. (Telegraph)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ni timu chache katika Ligi kuu ya soka zinazotaka kusaini mkataba na mshambulizi wa Atletico Madrid Fernando Torres mwenye umri wa miaka 34

Tottenham na West Ham wanamtaka mchezaji wa safu ya kati Barcelona Andre Gomes mwenye umri wa miaka 24- raia wa Ureno. (Mirror)

Meneja wa zamani wa Paris St-Germain Laurent Blanc analengwa na Chelsea, Everton pamoja na Lyon ikiwa timu hizo zitaamua kubadili meneja kwa msimu ujao. (Le10 Sport - in French)

Ni timu chache katika Ligi kuu ya soka zinazotaka zinazoonyesha ari ya kusiani mkataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Atletico Madrid Fernando Torres mwenye umri wa miaka 34 mwishoni mwa msimu . (Sports Illustrated)

Rais wa timu ya Roma James Pallotta ameomba radhi na akaahidi kulipa faini baada ya kuruka hadi ndani ya dimbwi la maji katika mji mkuu wa Italia alipokuwa akisherehekea ushindi wa timu yake dhidi ya Barcelona ilioiwezesha kuingia robo fainali katika michuano ya kuwania Ligi ya Championi. (Goal)

Mada zinazohusiana