Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 13.04.2018

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah
Image caption Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hakuna uwezekano wowote kwamba mshambuliaji wa Misri Mo Salah atauzwa mwisho wa msimu huu. (Daily Mail)

Tottenham inataka kumnunua beki wa West Ham na Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 Arthur Masuaku huku ikijiandaa kuondoka kwa beki Danny Rose (Sun)

Image caption Mkufunzi wa Tottenham hotspurs Mauricio Pochettino

Mkufunzi wa Tottenham hotspurs Mauricio Pochettino anasema kuwa mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 Harry Kane amekasirishwa kwa ukosoaji uliofuta baada ya hatua yake ya klabu hiyo kudai bao la pili la timu hiyo dhidi ya Stoke. (Telegraph)

Beki wa West Brom na Ireland , 30, Jonny Evans anatumai kujiunga na klabu ya Manchester City mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Image caption kocha wa ManCity Pep Guardiola anataka kusaini kiungo wa kati mmoja na winga.

Kwengineko kocha wa ManCity Pep Guardiola anataka kusaini kiungo wa kati mmoja na winga. (Times - subscription required)

Chelsea inapanga kumsajili mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri kuchukua mahala pake Antonio Conte mwisho wa msimu huu . (Mirror)

Image caption Chelsea inapanga kumsajili mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri kuchukua mahala pake Antonio Conte mwisho wa msimu huu . (Mirror)

Barcelona haitaharakisha kandarasi mpya na beki wake mwenye umri wa miaka 24 Samuel Umtiti. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkufunzi wa Sunderland Chris Coleman ametetea uamuzi wake wa kuzuia tiketi za mechi za nyumbani ili kujilinda dhidi ya mashabiki wa Newcastle kwa lengo la kuhakikisha kuwa timu hiyo haishushwi daraja. (Northern Echo)

Mshambuliaji wa Leicester na Algeria ,29, Islam Slimani huenda akaweka uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Newcastle kuwa mkataba wa kudumu (Leicester Mercury)

Image caption Harry Winks

Dau la Crystal Palace la £100m kuimarisha eneo moja la uwanja wa Selhurst Park limeungwa mkono na maafisa wa mipango . (Evening Standard)

Mchezaji wa Tottenham mwenye umri wa miaka 22 Harry Winks anapatiwa matibabu na wataalam nchini Qatar huku akitarajia kupona jeraha la kifundo cha mguu.. (Evening Standard)

Image caption Niko Kovac

Mkufunzi wa Eintracht Frankfurt na kocha wa zamani wa Croatia Niko Kovac anatarajiwa kusajiliwa kuwa mkufunzi mpya wa Bayern . (Kicker - in German)

Mchezaji wa Tottenham Danny Rose hatoshiriki katika mechi ya nyumbani dhidi ya Manchester City siku ya Jumamosi kutokana na jeraha la mguu.. (Daily Mail)

Mada zinazohusiana