Arsenal yanusurika kombe la Yuropa

Arsenal ambayo inaongoza kwa mabao katika kinyang'anyiro hicho haikushambulia hata mara moja katika dakika 70 za mwanzo na Laurent Kolscieny alipoteza nafasi ya wazi kabla ya Welbeck kufunga. Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Arsenal ambayo inaongoza kwa mabao katika kinyang'anyiro hicho haikushambulia hata mara moja katika dakika 70 za mwanzo na Laurent Kolscieny alipoteza nafasi ya wazi kabla ya Welbeck kufunga.

Arsenal ilitinga nusu fainali ya kombe la bara Yuropa kwa jumla ya mabao 6-3 dhidi ya CSKA Moscow licha ya sare ya 2-2 nchini Urusi.

Kikosi hicho cha Arsene Wenger kilikuwa nyuma 2-0 na chini ya presha wakati bao la Danny Welbeck la kipindi cha pili lilipowapatia ahueni.

Wenyeji walioongoza kupitia Fedor Chalov na Kirill Nababkin walikaribia kuwashangaza Arsenal kwa jumla ya mabao na kuongoza kwa bao la ugenini huku Petr Cech akilazimika kuokoa mkwaju wa adhabu wa Aleksandr Golovin pamoja na mkwaju wa Sergei Ignashevich.

Arsenal ambayo inaongoza kwa mabao katika kinyang'anyiro hicho haikushambulia hata mara moja katika dakika 70 za mwanzo na Laurent Kolscieny alipoteza nafasi ya wazi kabla ya Welbeck kufunga.

Bao la Aaron Ramsey kunako dakika za lala salama liliwavunja moyo CSKA na kuipatia fursa Arsenal kufuzu katika nusu fainali pamoja na Atletico Madrid, Marseille and Salzburg.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mohamed El-Neny alichaguliwa mchezaji bora katika mechi hiyo

Kikosi cha Viktor Goncharenko kilikuwa na ndoto ya kuwashangaza Arsenal wakati Chalov alipofunga bao la kwanza.

Lakini Arsenal iliompoteza Wilshere kupitia jeraha iliendelea kutawala mechi na kuonyesha mchezo mzurikabla ya kupata ushindi huo.

Mada zinazohusiana