Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 14.04.2018

Gareth Bale
Image caption Gareth Bale

Gareth Bale hakufurahia kutolewa wakati wa kipindi cha mapumziko katika mechi ya robo fainali ya Real Madrid nyumbani dhidi ya Juventus , lakini mshambuliaji huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 28 anataka kusalia katika klabu hiyo ya La Liga.(Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera hajui iwapo ataandikisha mkataba mpya katika uwanja wa Old Traford.

Image caption Anders Herrera

Raia huyo wa Uhispania 28 ana kandarasi na klabu hiyo ya ligi ya Uingereza hadi 2019. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Tottenham na West Ham wanawania kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona ,24,Andre Gomes. (Sport)

Everton inataka kumsajili kiungo wa kati wa Nantes na Ufaransa Kamal Bafounta. (L'Equipe - in French)

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Drinkwater

West Ham inataka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 Danny Drinkwater ambaye alijiunga na the Blues kwa kitita cha £35m last summer. (Telegraph)

Mkufunzi wa Barcelona Ernesto Valverde amemtetea nyota wa klabu hiyo Lionel Messi baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kukosolewa baada ya timu hiyo kubanduliwa katika kombe la vilabu bingwa .

Image caption Lionel Messi

Pia alikana kukosana na mchezaji huyo pamoja na beki Gerard Pique, 31, baada ya mechi hiyo.

Manchester City huenda wakatumia uwanja wao wa Etihad na Manchester United iwapo mipango wa kuurekebisha uwanja wa Old Traffotd itafanyika. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa Chelsea na Manchester United ziliongoza mpango wa kuanza kutumia teknolojia ya video ya VAR katika ligi ya Uingereza msimu ujao.. (Mirror)

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa sio wa kulaumiwa pekee kufuatia matokeo mabaya ya klabu hiyo kwa kuwa makosa yamefanywa na kila mtu katika klabu hiyo". (Mirror)

Image caption Antonia Conte

Hatma ya mkufunzi wa Arsenal Arsene katika klabu hiyo huenda ikategemea na kikosi chake iwpao kitaishinda klabu ya kaytika nusu fainali ya kombe la Yuropa (Telegraph)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 26, anaamini kwamba ushindi wa kombe la ligi ya Yuropa kutaisadia msimu wa Arsenal na kunedeleza uongozi wa Wenmhger katika klabu hiyo.

Mada zinazohusiana