Arsene Wenger akubali kuondoka Arsenal, amewacha sifa gani Afrika?

Arsene Wenger Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsene Wenger ndiye mkufunzi analiyehudumu kwa muda mrefu katika Premier League

Mkufunzi wa Arsenal amekubali kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Wenger amesema:

Baada ya kutafakari na kufanya mazungumzo na klabu , nahisi ni wakati muafaka kujiuzulu mwisho wa msimu huu.

Nashukuru kwa kupata fursa ya kuihudumia klabu hii kwa miaka mingi.

Niliongoza klabu hii na moyo wangu wote pamoja na maadili.

Nataka kuwashukuru wafanyikazi, wachezaji Mkurugenzi na mashabiki ambao wameifanya klabu hii kuwa maalum..

Nawaomba mashabiki wetu kuisaidia timu hii kumaliza msimu huu vizuri.

Kwa wapendwa wote wa Arsenal tunzeni maadili ya klabu hii.

'Naipenda na nitaishabikia maisha yangu yote'

Amesema Arsene Wenger katika taarifa yake.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Wenger na Jose Mourinho walikuwa kama 'pamba na moto'uwanjani .

Mmiliki wa klabu hiyo mwenye hisa nyingi Stan Kroenke alisema: Hii ni miongoni mwa siku ngumu zaidi katika miaka mingi ya mchezo huu.

Mojawapo ya sababu kuu ya kushirikiana na Arsenal ilikuwa kile kilicholetwa na Arsene Wenger ndani na nje. Uongozi wake wa muda mrefu na kile alichoweza kuiletea Arsenal hakiwezi kuafikiwa Alisema Kroenke.

Arsene Wenger anaacha sifa kubwa Afrika

Hivi maajuzi Arsene Wenger aliiambia BBC Africa kwamba t wachezaji wa kutoka Afrika wamekuwa na athari kubwa katika kazi yake katika miaka 20 iliyopita.

Ansema wachezaji wa Afrika wana arikubwa, ubunifu, wan anguvu, na wana ukakamavu ambao sio rahisi kupatikana katika soka.

Amewataja wachezaji wa Nigeria Nwako Kanu, wa Ivory Coast Kolo Toure na shujaa wa Liberia George Weah, aliyewasimamia katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na athari kubwa katika kazi yake kama kocha wa timu ya soka.

Wachezaji kadhaa wamechenga ufanisi katika soka ya kulipwa chini ya ukufunzi wake katika timu ya Arsenal.

Alishinda mataji matatu ya Premier, mataji 7 ya FA na kufanikisha timu kufuza kwa ligiya mabingwa kwa miaka 20 mtawalia.

Kwa mashabiki wengu wa soka, atakumbukwa kwa jukumu lake katika kuleta mageuzi katika mchezo huo England kwa mbinu tofauti.

Mada zinazohusiana