Wenger awasifu Nwanko Kanu, Kolo Toure na George Weah

Kanu
Image caption kanu

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger aliiambia BBC Africa kwamba wachezaji wa kutoka Afrika wamekuwa na athari kubwa katika kazi yake katika kipindi cha miaka 22 iliyopita.

Anasema wachezaji wa Afrika wana ari kubwa, ubunifu, wana nguvu, mbali na ukakamavu ambao sio rahisi kupatikana katika soka.

Amewataja wachezaji wa Nigeria Nwako Kanu, wa Ivory Coast Kolo Toure na shujaa wa Liberia George Weah, aliyewasimamia katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na athari kubwa katika kazi yake kama kocha wa timu ya soka.

Image caption George Weah

Wachezaji kadhaa wamechengia ufanisi katika soka ya kulipwa chini ya ukufunzi wake katika timu ya Arsenal.

Image caption Kolo Toure

Alishinda mataji matatu ya Premier, mataji 7 ya FA na kufanikisha timu kufuza kwa ligi ya mabingwa kwa miaka 20 mtawalia.

Kwa mashabiki wengi wa soka, atakumbukwa kwa jukumu lake katika kuleta mageuzi katika mchezo huo Uingereza kupitia mbinu tofauti.

Mada zinazohusiana