FA yaomba radhi kwa ujumbe wake wa mtandao wa Twitter

Harry Kane akichuana na Chris Smalling katika mchezo wa kombe la Fa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Kane akichuana na Chris Smalling katika mchezo wa kombe la Fa

Chama cha soka cha England FA, kimeomba radhi baada ya akaunti yake ya mtandao wa twitter kumdhihaki mshambuliaji Harry Kane, baada ya Tottenham kufungwa na Man United 2-1 katika nusu fainali ya michuano ya kombe la Fa.

Ujumbe uliowekwa katika mtandao wa Twitter , Ulionyesha beki wa Man United Chris Smalling,akiulizwa "Nani yuko kwenye mfuko wako? "na kukawa na kipande kifupi Smalling akijibu "Harry Kane".

Msemaji wa FA, amesema tayari wameandika barua kwa vilabu vyote viwili kuomba radhi kwa kosa hilo.

Hata hivyo, inaaminika ujumbe huu uliwavutia watu wengi kwa uhalisia wake wa kuwa umeandikwa katika ukurasa rasmi kutoka chama cha soka FA.

Klabu ya Tottenham wao hawajajibu chochote kuhusiana na jambo hilo, Kane alijidahidi kuisaidi timu yake katika mchezo huo wa nusu fainali licha ya kuwa ametoka katika maumivu ya siku za karibuni ya enka.