Mohamed Salah: Ilikuwaje akawa mchezaji nyota?

Mo Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mo Salah amefunga bao 43 kati ya mechi 48 kwa Liverpool kufikia sasa msimu huu.

Huku wachezaji wakisherehekea kwa fujo baada 4-0 dhidi ya ENPPI, kocha Said Al Shesheni aliangalia upande mmoja na kugundua kwamba mchezaji mmoja wa kikosi cha al-Mokawloon wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16 hakuwa akifurahia michuano iliokuwa Cairo.

Alikuwa akibubujikwa na machozi kwamba jina lake halikuwa katika orodha ya wafungaji mabao.

Akicheza kama beki wa kushoto ilikuwa vigumu kuchukua jukumu kubwa kama alivyotaka.

Akiwa mzaliwa wa eneo la Nagrig, kijiji kimoja kilichopo kilomita 130 Kaskazini mwa mji mkuu wa Misri, mchezaji huyo alilazimika kupitia tatizo la kusafiri kwa saa tisa kila siku mara nyengine akilazimika kutumia mabasi 10, ili kuweza kufika mazoezini mbali na kushiriki mechi.

Na baada ya kufurahishwa na ari ya kijana huyo Al Sheheni alimpatia fursa na kumpeleka safu ya mbele. Tangu wakati huo Mohammed Salah hajarudi nyuma tena.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji huyo wa Liverpool alilazimika kulipia uwanja mpya katika shule yake ya zamani

Habari hiyo ni jibu kwa swali ambalo limekuwa katika fikra za mashabiki wa soka duniani: Mchezaji ambaye hakuwa na athari yoyote kimchezo katika ligi kuu za Ulaya mara moja amekuwa mfungaji bora akilinganishwa na Lionel Messi na Christiano Ronaldo?

Katika soka inasaidia wakati mchezaji anapojikuta katika eneo analohitajika kuwa na katika wakati ufaao. Lakini ni watu wachache waliokuwa na hilo wakati Liverpool ilipotangaza usajili wa Salah kutoka klabu ya Itali ya Rome mwaka uliopita .

Kitita cha $55.7m kinaonekana kuwa cha juu kwa mchezaji ambaye alikuwa amefeli kuonyesha umahiri wake katika soka ya Uingereza baada ya kuhudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa Chelsea 2015.

Pia ni muhimu kuona kwamba Misri sio timu yenye umaarufu mkubwa katika soka duniani , ijapokuwa ina umaarufu mkubwa barani Afrika, baada ya kushinda taji la kombe la Afrika mara saba.

Lakini The Pharaoh wamecheza katika michuano miwili ya kombe la dunia 1934 na 1990 na hadi Salah alipoimarika, ilikuwa rahisi kutajwa kwa kuwa kipa Essam El-Hadary yuko katika harakati za kuwa mchezaji mkongwe zaidi kushirki katika kombe la dunia, wakati Misri iliporejea katika kinyang'anyiro hicho nchini Urusi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Misri imeshiriki katika michuano miwili pekee ya kombe la dunia lakini wamefaulu kushiriki Urusi 2018

Ni nini kilichofanyika kimakosa kwa Salah mapema alipocheza Uingereza? Kwanza Salah alishiriki katika ligi ya Switzerland, ambayo haina ushindani mkubwa kama ile ya Uingereza.

Akiwa Chelsea pia alikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji walioimarika na hakupata fursa za kutosha kuonyesha umahiri wake.

Raia huyo wa Misri alicheza mechi 19 kwa klabu hiyo ya London huku akianzishwa katika mechi tisa pekee. Ni mara mbili pekee alipocheza dakika zote 90. Salah baadaye alipelekwa kwa mkopo kwa vilabu vya Itali kabla ya kusainiwa na Roma kwa msimu wa 2015/16

Ni wakati huo ambapo Salah alionyesha umahiri wake na kufunga mabao 34 katika misimu miwili kabla ya kuelekea Liverpool.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Salah hakuwezi kufanya vizuri chini ya usimamizi wa Mourinho akiwa Chelsea: Alicheza mechi 19 na kufunga mabao 2 pekee

"Alikuwa mtoto alipowasili Chelsea na Chelsea ilikuwa na kikosi kizuri hivyobasi ilikuwa vigumu'' , alisema mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp akizungumza na runinga ya Ujerumani wiki hii.

"Nadhani sote lazima tukubaliane kwamba Jos Mourinho ni kocha mzuri kwa hivyo mara nyengine mambo huwa hivyo .Kwa hivyo iwapo haiwezekani jiondoe ujaribu tena na hivyo ndivyo ilivyokuwa na Mohamed."

Katika ziara ya hivi karibuni Anfield, Mourinho, ambaye sasa ni mkufunzi wa Manchester United alionekana akimkumbatia raia huyo wa Misri.

Na mahojiano na ESPN Brasil yaliorushwa hewani Jumapili iliopita, raia huyo wa Ureno alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na mchezaji huyo.

''Ni mimi ndio niliyemsaini Salah na uamuzi wa kumuuza haukuwa wangu, bali ulikuwa wa Chelsea''.

''Ni mtu mzuri , lakini alikuwa mdogo na hakuwa amejiandaa kimaungo na kifikra wakati alipwasili. Pia alipata utamaduni tofauti. Nafurahi sana kumujona anaendelea vyema , hususan kwa sababu hajafunga dhidi ya Unite'', alifanya mzaha.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mambo yamekuwa tofauti kwake Liverpool

Inawezekana kwamba magoli aliyofunga katika msimu wa 2017/18 yalipita kiwango ambacho mchezaji huyo alikuwa ametaka kuafikia. Katika mechi 48 alizochezea Liverpool katika mashindano yote, raia huyo wa Misri alifunga mabao 43 na kusaidia pasi za baoa 15.

Amekuwa nyota katika kombe la vilabu bingwa Ulaya ambapo ameisaidia Liverpool kukaribia kufika fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu 2007.

Raia huyo wa Misri ni baraka kwa aina ya mchezo wa Klopp kwa kasi na mashambulio.

Mbali na mafanikio yake , Salah anaweza kufanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika kushinda taji la mfungaji bora Ulaya, taji analokabidhiwa mfungaji bora katika ligi ya Ulaya.

Na msimu wa Salah hautakamilika katika wikendi ya mwisho ya ligi ya premia. Timu ya taifa imefanikiwa kufuzu katika kombe la dunia la 2018 ikiwa ni la kwanza katika kipindi cha miaka 28 baada ya kampeni ya kuwania kufuzu ambapo Salah alifunga mabao matano kati ya manane huku akitoa usaidizi wa mabao mawili.

Ushujaa wake ulihusisha penalti ya dakika 94 dhidi ya Congo ambayo ilikamilisha kufuzu kwa taifa hilo katika kombe la dunia .

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Salah alifunga mabao matano kati ya magoli ya Misri katika kombe la kombe la dunia

Na kudhania kwamba kuimarika kwake kulianza kwa bahati .Mnamo mwezi machi 2012 , soka ya Misri ilikuwa imedorora: ligi ya taifa hilo ilisitishwa kutokana na janga la uwanja wa Port Said - maandamano ambayo mapema takriban watu 70 walifariki huku wengine 500 wakijeruhiwa.

Huku wakitafuta kushiriki katika mechi kwa maandalizi ya michezo ya Olimpiki mjini London , timu hiyo ya Misri yenye wachezaji wasiozdi umri ya miaka U-23 walipanga mechi za kirafiki hidi ya vilabu za Ulaya.

Mojawapo ni klabu ya Uswizi ya Basel, ambaye rais wake, Bernhard Heusler, alimsajili Salah hapo kwa hapo.

"Kulikuwa na baridi kali lakini alionyesha mchezo mzuri .Alicheza kipindi cha pili pekee lakini sijaona mchezaji mwenye kasi katika maisha yangu yote'',alisema Heusler

Wachezaji wenza wa Basel wanakumbuka kwamba Salah hakuchezshwa mara moja. Katika mwaka wake wa kwanza katika klabu hiyo mchezaji huyo alitumiwa kama mchezaji wa ziada na ni katika mechi 10 pekee kati ya 29 ambapo alicheza kwa zaidi ya saa moja.

Mchezaji mwenza Philipp Degen, aliambia Sky Sports habari kuhusu Salah alivyomshangaza kila mtu baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Chelsea katika mechi ya kombe la vilabu bingwa .

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Salah alijiunga na Basel mwaka 2012 baada ya kucheza kipindi kimoja pekee ya mechi dhidi ya timu ya Usiwzi

"Tulijaribu kumpa hongera lakini hakukubali. Anasema kuwa alipiga nje mikwaju sita na ni wa saba tu pekee kwa kuwa klabu ilimuamini. Umaruufu wake pia unatokana na kuwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu.

Anapendwa sana nchini Misri wakati ambapo taifa hilo limegawanyika katika misingi ya kisiasa ilioanzishwa mika michache iliopita na maandamano ya Uarbuni na mapinduzi ya 2013, lakini Salah anapenda mizizi yake.

Amelipia ujenzi wa shule na hospitali na kuweka jina lake katika mashirika ya hisani ikiwemo kuchangisha $280,000 kwa hazina ya srikali inayolenga kuimarisha kiuchumi familia za Wamisri masikini.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji huyo ni shujaa wa taifa lake la Misri

Utata unaozunguka jina la Zalah unashirikisha madai kwamba alikataa kusalimiana na wachezaji kutoka klabu ya Israel ya Maccabi Tel-Aviv katika mechi dhidi ya Basel mwaka 2013 - alienda kubadili viatu vyake kabla ya mechi kuanza. wakati huo raia wenmgi wa Misri walikuwa wamepinga vitendo vyake na hata kumtaka mchezaji huyo kutoshirikishjwa katika mechiya ugenini ya Israel.

Hathivyo mbali na kuzomwa na mashabiki wa Maccabi Salah alicheza mechi ya ugenini na kufanikiwa kufunga bao.

Wiki iliopita baada ya raia huyo wa Misri kuisaidia Liverpool kushinda 5-2 dhidi ya Roma katika kombe la vilabu bingwa, waziri wa ulinzi Avigdor Lieberman alituma ujumbe wa twitter kwamba atampigia mkuu wa utumishi wa umma kumsaini Mohammed salah kwa mktaba wa kudumu na jeshi la Israel.