Fainali ya ubingwa Ulaya: Je mashabiki wa Liverpool na Real Madrid watarajie nini Kiev?

Shabiki wa Liverpool Haki miliki ya picha Getty Images

Bustani za maua, na gwaride la wanajeshi 3000 ndiyo baadhi ya mambo watakayo karibishwa nayo mashabiki wa Liverpool na Real Madrid wakati timu hizo mbili kubwa zitakapokutana katika fainali za ligi ya Ubingwa katika uwanja wa Olympic Stadium mnamo Mei 26.

Uwanja huo - umejizolea umaarufu kwa kuwa mwenyeji wa baadhiya mechi za soka katika mashindano ya Olimpiki Moscow mnamo 1980 .

Una takriban viti 70,050 licha ya kwamba kiwango cha mashabiki watakaoruhusiwa katika fainali hiyo ni 63,000.

Haki miliki ya picha UNIAN
Image caption Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev utakuwa mwenyeji wa fainali ya kwanza ya ligi ya ubingwa nchini Ukraine

Vilabu vyote vimepewa takriban tiketi 16 500 kwa hivyo jumla ya mashabiki 33,000 wa Liverpool na wa Real Madrid wanatarajiwa kusafiri kuelekea katika mji mkuu huo wa Ukraine - na pia mashabiki wa Wolfsburg na Lyon kwa fainali ya ligi hiyo kwa wanawake siku mbili kabla ya hapo itakayochezwa katika uwanja mdogo wa Dynamo.

Meya wa mji wa Kiev Vitali Klitschko - bingwa mara tatu uzani mzito wa masumbwi amesema anatarajia hadi watalii 100,000 mwishoni mwa juma.

"Kwa kipindi cha fainali hiyo, kando na vikosi vya polisi mjini Kiev na maeneo mengine, wanajeshi 3000 watasaidia katika kuhakikisha utulivu," amesema naibu waziri wa mambo ya ndani Serhiy Yarovyi.

Image caption Uwanja wa Kontraktova ni mojawapo ya vivutio vikuu Kiev

Usafiri na malazi je?

Uwanja wa ndege mjini humo Borispol unatarajia ndege 100 za ziada mwishoni mwa juma.

Utafunga mojawapo wa njia kuu za uwanja huo ili kukabiliana ongezeko hilo, na kuruhusu njia nyingine kutumika kama maeneo ya ndege kusubiri.

Katika baadhi ya ndege ni marufuku kubeba mizigo ili kuharakisha kushuka kwa abiria.

Bei za kukodisha hoteli pia zinatarajiwa kupanda.

Mpaka sasa takwimu zinaonyesha 98% ya malazi katika hoteli yamekodishwa.

Haki miliki ya picha JEAN-CHRISTOPHE BOTT
Image caption Kikosi Shevchenko itakabiliana na Kikosi Klitschko katika mechi ya watu maarufu

Eneo kuu la kivutio linalojulikana kama 'kijiji cha mabingwa', lipo katika mtaa wa kati kati wa Khreshchatyk. Kutakuwa na mechi ndogo ya watu mashuhuri kati ya marafaiki wa meya Klitschko na mshambuliaji bingwa wa Ukrain Andriy Shevchenko.

Kila kijiji cha mji huo kinapanga kuwa na mpangilio wa maua na michoro na sanaa za aina nyingine, na Kibofu kikubwa kilicho mfano wa taji kuu la ligi hiyo ya ubingwa.

Ukarabati mkubwa umefanywa wa uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kuwekwa kamera za CCTV vipaza sauti na taa pamoja na kutengwa sehemu maalum ya waandishi habari.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii