Luyanda Ntshangase afariki dunia

South Afrika Haki miliki ya picha Maritzburg United
Image caption Mshambuliaji wa timu ya Maritzburg United Luyanda Ntshangase amefariki dunia

Mwanasoka nchini Afrika Kusini ambaye alipigwa na radi wakati wa mechi amefia hospitalini, klabu yake imethibitisha.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Maritzburg United Luyanda Ntshangase, aliyekuwa na umri wa miaka 21, alikuwa katika hali mahututi tangu alipojeruhiwa katika mchezo wa kirafiki tarehe 1 Machi.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa facebook wa klabu hiyo, imemuelezea mchezaji huyo kama miongoni mwa nyota mchanga aliyekuwa aking'ara na kuja kwa kasi kwenye ulimwengu wa soka la nchi hiyo na kwamba klabu hiyo iko kwenye majonzi mazito kufuatia kifo chake.

"Sisi tuna huzuni sana kuhusu kumpoteza Luyanda, mchezaji mchanga mzuri na mwenye uwezo mkubwa," alisema mwenyekiti wa Maritzburg Farook Kadodia katika taarifa hiyo.

"Kwa niaba ya klabu ya Soka ya Maritzburg United, tunataka kuonesha na kuwapa faraja zetu kwa familia ya Ntshangase."

Timu hiyo ya Maritzburg United iko kwenye daraja la nne katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Ntshangase ameibuka kwa ugumu katika soka na kujitutumua katika mchezo wake wa kwanza timu dhidi ya Kaizer Chiefs misimu miwili iliyopita.

vyombo vya habari nchini Afrika kusini vinaarifu kuwa mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliopigwa na mwali wa radi wakati wa mechi mjini KwaZulu-Natal, majeruhi wawili waliumia kidogo ingawa Ntshangase aliungua vibaya upande wa kifuani .

Vifo vya wachezaji huyo kwa ajali ya radi hii si mara ya kwanza kwani hii ni mara ya tatu kuikumba timu hiyo ya Maritzburg United katika miaka ya hivi karibuni.

Miongoni mwa waliopoteza uhaki kwa njia ya ajali tofauti ni Mondli Cele,aliyekuwa na miaka 27, na Mlondi Dlamini, 20, wote wawili walikufa kwa ajali za gari tofauti mmoja mwaka 2016 na mwingine 2017 .