Djokovic amtambia Nishikori Michuano ya Madrid

Novack Djokovic ashinda raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Madrid Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Novack Djokovic ashinda raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Madrid

Nyota namba kumi na mbili kwa ubora duniani kwa mchezo wa tenesi, Novack Djokovic, ameanza vyema michuano ya wazi wa Madrid kwa kumfunga Kei Nishikori.

Djokovic alishinda kwa seti mbili, za 7-5 6-4, baada ya ushindi huo mchezaji huyo akasema ushindi huo unamrejeshea kujiamini baada kushindwa kufika robo fainali katika mashindano matano tofauti yaliyopita toka alipotoka kwenye majeraha mwezi Januari.

Feliciano Lopez nae alipata ushindi wa seti mbili ya 7-6 na 6-3 dhidi ya Pablo Andujar, Gael Monfils akamtambia Nikoloz Basilashvili kwa kumfunga kwa 6-2 na 6-3.

Kwa upande wa wanawake Maria Sharapova aliibuka kidedea kwa kumshinda Irina-Camelia Begu kwa seti mbili za 7-5 na 6-1, Caroline Wozniacki akamshinda Ashleigh Barty kwa 6-2 na 6-4.

Karolina Pliskova aliibuka na ushindi wa seti mbili dhidi ya Victoria Azarenka, Pliskova alisinda kwa 6-2 kisha akapoteza kwa 6-1 na mwisho akashinda kwa 7-5.