Manchester United walipwa zaidi ya Manchester City mapato ya Ligi ya Premia Uingereza

Manchester United striker Romelu Lukaku celebrates Haki miliki ya picha Rex Features

Manchester United walipata pesa nyingi kuliko mabingwa wa ligi Manchester City kutoka kwenye Ligi ya Premia msimu uliomalizika majuzi, licha ya City kufana zaidi na hata kuweka rekodi.

United, waliomaliza wa pili, walipokea £149.77m, £328,491 zaidi ya City.

United walilipwa pesa zaidi kwa sababu kuna mechi zao mbili zaidi ambazo zilionyesha moja kwa moja kwenye runinga Uingereza - hii ina maana kwamba pesa walizolipwa kutokana na uwanja wao na huduma nyingine zilikuwa £2.26m zaidi.

Kwa jumla, klabu za Ligi ya Premia zilipokea £2.42bn, £2.1m zaidi kuliko msimu uliopita.

United chini ya meneja wao Jose Mourinho mechi zao zilizoonyeshwa kwenye runinga Uingereza msimu huu zilikuwa 28, sawa na zilizooneshwa za Liverpool na Arsenal. Hata hivyo, zilizoonyeshwa za City zilikuwa 26.

Malipo ya jumla kwa klabu hutokana na mapato kutoka kwa haki za utangazaji wa mechi kwenye runinga Uingereza (ambayo asilimia 50 yake hugawanywa kwa njia sawa kwa klabu zote. Asilimia 25% ya mapato yaliyosalia hugawanywa kwa kuzingatia mechi ambazo zimeonyeshwa moja kwa moja kwenye runinga, na asilimia 25 kwa kuzingatia nafasi ya klabu kwenye jedwali), mapato kutoka kwa shughuli nyingine za kibiashara na mapato kutoka kwa haki za utangazaji wa mechi kimataifa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester City walimaliza ligi wakiwa na alama 100, ambayo ni rekodi

City walipokea £38.63m kwa sababu ya kushinda ligi, £1.93m zaidi ya United waliomaliza wa pili.

Malipo kwa klabu za Ligi ya Premia 2017-18
Klabu (kwa kufuata nafasi ligini mwisho wa msimu) Idadi ya mechi zilizoonyeshwa moja kwa moja runingani Uingereza Pesa zilizotokana na nafasi kwenye ligi Malipo ya jumla
Manchester City 26 £38.63m £149.44m
Manchester United 28 £36.69m £149.77m
Tottenham 25 £34.76m £144.45m
Liverpool 28 £32.83m £145.90m
Chelsea 26 £30.90m £141.71m
Arsenal 28 £28.97m £142.04m
Burnley 10 £27.04m £119.77m
Everton 19 £25.11m £128.01m
Leicester 12 £23.18m £118.17m
Newcastle 18 £21.24m £123.02m
Crystal Palace 12 £19.31m £114.31m
Bournemouth 11 £17.38m £111.25m
West Ham 17 £15.45m £116.09m
Watford 10 £13.52m £106.25m
Brighton 13 £11.59m £107.71m
Huddersfield 10 £9.66m £102.39m
Southampton 16 £7.73m £107.24m
Swansea 10 £5.79m £98.53m
Stoke 12 £3.86m £98.86m
West Brom 10 £1.93m £94.67m

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii