Unai Emery kupewa mikoba ya Wenger Arsenal

Unai Emery anatarajiwa kupewa kazi ya kuwa meneja mpya wa Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Unai Emery anatarajiwa kupewa kazi ya kuwa meneja mpya wa Arsenal

Klabu ya Arsenal inatarajiwa wiki hii itamtangaza Unai Emery,kuwa meneja mpya wa klabu hiyo kuchukua mikoba ya Arsene Wenger.

Emery aliiacha na klabu yake ya Psg, mwanzoni mwa mwezi huu na alikuwa jijini London, jana jumatatu, kufanya mazungumzo na klabu ya Arsenal ya kuwa meneja mpya wa washika mitutu hao wa London.

Meneja huyu raia wa Hispania, mwenye umri wa miaka 46,aliisaidia klabu ya Psg, kutwaa mataji matatu katika msimu ulimalizika katikati ya mwezi huu na nafasi yake katika miamba hao wa Ufaransa imechukuliwa na Thomas Tuchel.

Kwa siku za karibuni kiungo wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ndio alitajwa angepewa jukumu la kupewa kazi ya umeneja ya kuwaongoza Arsenal baada ya miaka 22, ya kuongozwa na Arsene Wenger.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Santi Cazorla anaondoka katika timu ya Arsenal

Wakati huo huo kiungo wa Arsenal Santi Cazorla anaondoka klabuni hapo msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake, Cazorla ameichezea timu yake jumla ya michezo 180 toka alipojiunga na klabu hiyo mwak 2012 akitokea Malaga.