Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.05.2018

Neymar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa PSG , Neymar

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, amesema wazi wazi anatataka kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto , mwaka mmoja baada ya Mbrazil huyo kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa. (Goal)

Chelsea wamemuorodhesha mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, miongoni mwa wanaowataka kuwasajili msimu huu. (Telegraph)

Manchester United wanamatamanio ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Willian, 29, msimu huu wa uhamisho. (Sky Sports)

Lakini Manchester United wako tayari kujiondoa kwa uhamisho wa £53m wa Shakhtar Donetsk na kiungo wa kati wa Brazil Fred ,25. (Metro)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Manchester United Anthony Martial, 22, ananyemelewa na mahasimu wao wa ligi ya Premia Tottenham. (London Evening Standard)

Barcelona wanapanga kusamjili mshambuliaji wa Spurs Reo Griffiths katika uhamisho wa msimu huu wa joto. (Star)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Leicester Riyad Mahrez

Manchester City wanataka kumsajili winga wa Leicester Riyad Mahrez ,27, baada ya kumkosa raia huyo wa Algeria katika uhamizo wa mwezi January. (Manchester Evening News)

Hata hivyo uhamisho wa Mahrez kuelekea kaskazini Maghribi uligonga mwamba kutokana na ugumu wa malipo ya ada kwa ajenti wake. (Leicester Mercury)

Meneja wa Napoli Maurizio Sarri, anaoneka kuihamia Chelsea baada ya rais wa klabu hiyo ya Italia Aurelio de Laurentiis kukutana na Carlo Ancelotti kwa mazungumzo ya kumtaka yeye kuchukua nafasi ya Sarri. (Evening Standard)

Meneja wa Fulham Slavisa Jokanovic amejitokeza kwa ghafla kama mgombea anayetaka kazi ya umeneja kwa klabu ya Chelsea. (Express)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anamnyemelea Muingereza mmoja kati ya Waingereza wawili msimu huu, Jamaal Lascelles, 24 wa NewCastle au James Tarkowski,Burnley. (Independent)

Brighton wako karibu kukamilisha mkataba wa mchezaji wa kimataifa wa Nigeria Leon Balogun, 29, kutoka klabu ya Ujerumani ,Mainz. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Defenda wa Southampton Maya Yoshida

Defenda wa Southampton Maya Yoshida, 29,atasalia na klabu ya pwani mashariki licha ya mabingwa wa ligi ya Saudi Arabia Al Hilal kuwa na matamanio ya kumsajili. (Daily Echo)

Ipswich imemuhoji kiungo wa kati wa zamani wa England na Chelsea , Frank Lampard kuhusiana na pengo la umeneja kwenye klabu yao. (Mirror)

Jose Mourihno amemteuwa Kieran McKenna kutoka chuo cha mafunzo cha wafanyikazi wa klabu ya Manchester United kama meneja msaidizi wa tatu ili kuchua nafasi ya meneja msaidizi anayeondoka Rui Faria. (Daily Record)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlinda lango guli wa Juventus na Italia Gianluigi Buffon,

Mlinda lango guli wa Juventus na Italia Gianluigi Buffon, 40, yuko karibu kukubali mkataba wa kuihamia klabu ya mabingwa wa Ufaransa ya Paris St-Germain. (Mail)

Wolves wanampango wa kumsajili beki Mfaransa wa Marseille Bouna Sarr, 26 na kiungo wa kati raia wa Cameroon Andre-Frank Zambo Anguissa, 22. (Birmingham Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Difenda wa Aston Villa John Terry

Difenda wa Aston Villa John Terry ataiwachia klabu hiyo kuamua uhamisho wake msimu huu huku maombi kutoka kwa ligi kubwa za soka na Ligi Kuu ya Uchina yakitarajiwa. (Mirror)

Mmiliki wa klabu ya Sunderland Stewart Donald amesema kwamba klabu hiyo itamteuwa Chris Coleman kwa mara nyengine kama meneja, wiki tatu baada ya kumpiga kalamu meneja huyo. (Guardian)