Manuel Pellegrini atangazwa Meneja wa West Ham

Manuel Pellegrini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manuel Pellegrini ataidhinishwa kama meneja wa West Ham leo Jumane.

Manuel Pellegrini ameidhinishwa kama meneja wa West Ham.

Pellegerini 64, ambaye ni meneja wa zamani wa Manchester City na Real Madrid alisafiri kufanya mazungumzo baada ya kuacha kazi yake huko Hebei China Fortune mwishoni wa wiki.

Makubaliano ya mwisho yaliafikiwa jana Jumatatu usiku na kumwezesha Pellegerini kurejea katika Premier League.

Anachukua mahala pake David Moyes, ambaye aliachwa kuondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake na baada ya kuongoza Hammers kumaliza katika nafasi ya 13.

Pellegrini raia wa Chile ataungana na naibu wake Reuben Cousillas mjini London.

West Ham ilikuwa na mpango wa kumuajiri meneja wa Newcastle United Rafael Benitez, lakini kwa haraka wakasema kuwa ingekuwa vigumu kwa raia huyo wa Uhispania kuondoka St James' Park.

Pellegrini ambaye alikuwa analipwa mshahara mnono huko China, alikubali kuchukua mshahara wa chini kuchukua nafasi hiyo lakini hata hivyo atakuwa meneja ambaye amelipwa pesa nyingi zaidi katika historia ya West Ham.

Mwenyekiti David Sullivan awali alikuwa amesema alikuwa na nia ya kumuajiri mtu mwenye ujuzi wa juu.

Ana matumaini kwa Pellegrini ambaye alishinda Premier League mwaka 013-14 na mataji mawili ya EFL wakati wa kipindi chake cha miaka mitatu akiwa na Manchester City, pamoja na kufuzu kwa nusu fainali kwa ligi kuu ya mabigwa katika historia yake anaweza kuleta mabadiliko West Ham.