Ujumbe wa Arsenal wazuka na kupotea katika mtandao wa Emery, kulikoni?

Unai Emery screengrab
Maelezo ya picha,

Picha hiyo ilizuka katika mtandao rasmi wa meneja huyo kabla ya kuondolewa muda mfupi baadaye

Mtandao rasmi wa Unai Emery umeweka picha iliyo na ujumbe: "Nasikia fahari kuwa katika familia ya Arsenal."

Meneja huyo wa zamani wa Paris St-Germain manager anatarajiwa kuzinduliwa rasmi kama mrithi wa Arsene Wenger wiki hii.

Klabu hiyo ya London bado haijathibitisha kuwa Emery ndiye kocha mpya.

Lakini picha ya Emery iliyoambatana na ujumbe huo na nembo ya Arsenal iliwekwa kabla ya muda mfupi badaye kuondolewa.

Haijulikani kama picha hiyo iliwekwa kimakosa au ni kazi ya wadukuzi.

Mtandao huo www.unai-emery.com - unaohusishwa na akaunti ya Twitter ya raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 46 - baadaye ulikuwa unaonyesha kuwa na hitilifu kwa waliojaribu kuufungua.

Emery aliondoka PSG mwezi huu baada ya kuhudumu kwa miaka miwili ambapo alishinda taji la ligi na vikombe vinee vya mashindano ya nyumbani.

Awali aliwaongoza Sevilla kupata ushindi wa mara atatu latika ligi ya Uropa kati ya 2014 na 2016.

Wenger aliodnoka Arsenal mwezi huu baadaya kuhudumu kwa miaka 22.