Liverpool v Real madrid: Uwanja ambao Cristiano Ronaldo na Mo Salah watakutana

Uwanja wa Taifa wa Olimpiyskiy mjini Kiev utakuwa mwenyeji wa fainali inasubiriwa kwa hamu na ghamu ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Liverpool na Real Madrid Jumamosi.

Uwanja huo umekarabatiwa majuzi kwa gharama ya $3.6m kwa ajili ya fainali hiyo.

Ndio uwanja ambao utawakutanisha Cristiano Ronaldo na Mo Salah.