Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 26.05.2018

Isco

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Isco

Manchester United wana nia ya kuipa Real Madrid ofa ya pauni milioni 70 kwa kiungo wake wa safu ya kati raia wa Uhispania mwenye miaka 26 Isco. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mshambulizi wa Chelsea Michy Batshuayi anasema hawezi kuamua hadi baada ya kombe la dunia ikiwa atarudi Stamford Bridge. Rais huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 alitumikia duru ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo huko Borussia Dortmund.(Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Anthony Martial

Tottenham itaiomba Manchester United mshambuliaji raia wa Ufaransa Anthony Martial 22, ikiwa mlinzi raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 29 atahamia Tottenham.

Chelsea inaweza kumtoa mshambulili raia wa Uhuspania Alvaro Morata 25, kwa Inter Milan ili kumdilisha na mshambulizi raia wa Argentina Mauro Icardi, 25. (Il Messaggero, via Mail)

Arsenal na Chelsea watapata ushindani kutoka Napoli na Borussia Dortmund kumpata kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast Jean-Michael Seri, 26. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marco Asensio

Maajenti wa Marco Asensio wanasema Real Madrid wamekataa ofa mbili kutoka klabu za Premier League za thamani ya hadi pauni milioni 130 kwa mshambulizi mhispania mwenye miaka 22 ambaye amehusishwa na Manchester United na Chelsea. (Independent)

West Ham wako nafasi nzuri kumsaini mlinzi wa Barcelona Marlon. Mbrazili hiyo wa miaka 22 ambaye anacheza kwa mkopo wa miaka miwili na klabua Nice pia anawindwa na Leicester. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Riyad Mahrez

Manchester City wanataka kuwasaini kiungo wa kati wa Italia Jorginho kutoka Napoli, wing'a wa Leicester raia wa Algeria Riyad Mahrez, 27 na mshambuliaji wa Bayer Leverkusen raia wa Jamaica Leon Bailey. (Manchester Evening News)

Arsenal wanakabiliwa na upinzani kutoka RB Leipzig kumsaini wing'a wa Chelsea raia wa Brazil Kenedy, 22. (Goal)

Manchester United walikwa na matumaini ya kumsaini beki wa Juvemntus raia wa Brazil Alex Sandro, lakini mchezaji huyo wa miak 27 anatarajiwa kufanya mazungumzo wiki ijayo kubaki nchini Italia. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameweka tayari pauni milioni 30 kumnunua beki wa Valencia Joao Cancelo. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno mwenye umri wa maika 23 akiwa Inter Milan msimu uliopita kwa mkopo. (Mirror)

Chelsea wanakabiliwa na usindani kutoka kwa Zenit St Petersburg ya Urusi kwa meneja Maurizio Sarri. Meneja huyo wa Napoli anaonwa kama anayeweza kuchukua mahala pake Antonio Conte huko Stamford Bridge. (Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Emre Can

Kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 24, atajiunga na Juventus mwisho mwa mwezi huu huku mkurugenzi mkuu wa mabingwa hao wa Italia Giuseppe Marotta akisema anataka kukamilisha mpango huo ndani ya siku 10. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Manchester United wana nia kulipa pauni milioni 79 kumsaini wing'a Douglas Costa kutoka Bayern Munich. Mchezaji huyo raia wa Brazil mwennye miaka 27 yuko kwa mkopo huko Juventus na mabingwa hao wa Italia wana uamuzi wa kumsaini kabisa. (Sun)

Kwingineko United hawama uhakika ikiwa watamwinda kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, baada ya klabu hiyo ya Italia kutangaza bei ya mchezaji huo kuwa pauni milioni 87.5 kwa raia huyo Serbia. (Mail)