Fainali klabu bingwa Ulaya: Real Madrid wataweza kuizuia mishale ya Liverpool?

Liverpool's Mo Salah scores in the Champions League semi final against Roma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Liverpool have scored 40 goals in 12 Champions League matches this season. Mohamed Salah (10), Roberto Firmino (10) and Sadio Mane (9) have scored 29 of them

Kila mmoja atatarajia mashambulizi makali zaid kutoka Liverpool wakati wa fainali la klabu bingwa Ulaya lakini kile hatufahamu ni jinsi Real Madri itakabiliana na hali hiyo.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp hana nia ya kubadilsha mbinu za kikosi chake cha 4-3-3 kwenye mechi ya leo Jumamosi na kama kutakuwepo na majeraha inamaanisha kuwa hatakuwa na mbinu tofauti pia wa wachezaji.

Kwa upande mwingine meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane ana maauzi makubwa ya kufanya kuhusu ni yupi anayamweka kwenye kikosi cha mechi ya Kiev.

Zidane amekuwa na nyakati msimu huu ambapo kikosi chake kimekuwa na wakati mgumu hasa Ulaya lakini licha ya hilo amefanikiwa.

Ameifikisha Real fainali sio kwa kuangazia pande moja lakini kwa kuwasoma sana wapinzani.

Kwa kufanya hilo na kubadilisha jinsi Real wanacheza kutokana na ni nani wanacheza naye, ameonyesha kuwa sio kocha anayetuma kikosi chake na kukiambia kucheza vile wanacheza licha ya wachezaji wazuri alio nao.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

Kikosi cha Liverpool kilichocheza nusu fainali na Roma kinatarajiwa kuanza huko Kiev

Real lazima iwakabili vilivyo washambuliaji watatu wa Liverpool

Moja ya vita vikali zaid vitakuwa kutoka Mohamed Salah ambaye ni mshambuliaji hatari zaidi duniani dhidi ya mlinzi wa Real Mbrazil Marcelo.

Marcelo ni muhimu sana kwa Real lakini kumwezesha kucheza vizuri zaidi bila ya kuiacha safu ya ulinzi na hatarai kutoka Liverpol ni jamboa litasababisha Zinade kuamua mfumo ambao atautumia.

Amekuwa mwangalifu akicheza na timu ambayo hucheza kwa kushambulia kwa ghafla kama Liverpool na huenda akaitumia mbinu sawa na hiyo.

Zinade pia huenda akafikiria kuwa ikiwa Marcelo atacheza mbele ataupa upande wake ulinzi zaidi akisaidiana na safu ya kati kama Mateo Kovacic na katika mfumo wa 4-4-2 sawa na alivyofanya wakati wa duru ya pili ya ushindi wake dhidi ya PSG.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

Zidane alitumia 4-4-2 huko Paris akicheza na Paris St-Germain.