Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 27.05.2018

Joe Hart akiwania mpira
Maelezo ya picha,

Joe Hart akiwania mpira

Mlinda mlango wa Manchester City Joe Hart, 31, ameibuka kuwa chaguo la Manchester United kusaidia na David de Gea, 27. Baada ya meneja Jose Mourinho kuona mlinda mlango namba mbili Sergio Romero, 31 anataka kuondoka. (sun).

Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, anatarajia kurejea Japan kuendelea na kazi yake ya ukocha.(Mail on Sunday).

Juventus imezungumza na Atletico Madrid kuhusu uwezekano wa kumsajili mlinzi mwenye asili ya Uruguay, Diego Godin, 32.(Calciomercato)

Wakati huo huo beki wa kulia wa Juve Stephan Lichtsteiner, 34, anajiandaa kujiunga na Arsenal bila malipo ya uhamisho.(London Evening Standard)

Meneja Steve Bruce amemtaka kiungo wa kati Jack Grealish, 22, kubaki Aston Villa kwa msimu mwingine baada ya fainali ya michuano ya mabingwa.(Express and Star)

Paris St-Germain mshambuliaji Neymar, 26,amerejea kauli yake kuwa ana shauku siku moja acheze chini ya meneja Pep Guardiola.(ESPN Brasil, in Portuguese)

Maelezo ya picha,

Neymar anatamani kufanya kazi chini ya Pep Guardiola

Everton inatarajia kutumia mwanya wa timu za Manchester United na Manchester City kukaa kimya kusajili mlinzi wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, 27. (sun).

Wakati huo huo Rose ni miongoni mwa walinzi watatu wa kushoto ambao wapo kwenye rada za Manchester United akiwepo pia beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 27, na Elseid Hysaj, 24 wa Napoli. Uhamisho huo unatarajiwa kuona Matteo Darmian, 28, akienda Juventus. (Gazzetto dello Sport).

Hata hivyo, Paris St-Germain iko kwenye ushindani na Manchester United kunyakua saini ya Sandro ingawa United imeripotiwa kuanza mazungumzo na wakala wa mlinzi huyo mwenye asili ya Brazili.(Manchester Evening News)

Mwenyekiti wa klabu ya Ostersunds ya Sweden Daniel Kindberg na meneja wa timu hiyo Graham Potter wamesema wamepokea ombi la kuiongoza klabu ya Swansea City, licha ya kuwa hakuna mazungumzo ambayo yamefanyika mpaka sasa. (Wales Online).

Mshambuliaji wa Swansea,Jordan Ayew, 28, amekuwa akizungumziwa na Celtic, kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo.(Daily Record)

Manchester City inakamilisha uhamisho wa kiungo mshambuliaji Riyad Mahrez,27 kutoka Leicester City kwa kitita cha Pauni milioni 75. (Mail on Sunday)

Maelezo ya picha,

Riyad Mahrez

West Ham inaripotiwa kuongoza katika mbio za kumsajili mlinzi wa Barcelona, Marlon Santos, 22, ambaye kwa sasayuko kwa mkopo na klabu ya Nice.(Mundo Deportivo, in Spanish)

Borussia Dortmund imekuwa na mazungumzo na Chelsea kuhusu ombi la kumsajili Michy Batshuayi. mshambuliaji huyo alitumia nusu ya pili ya msimu kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ujerumani.(Mail on Sunday)