Ronaldo kutangaza mustakabali wake punde

Ronaldo amefunga mabao 120 kwenye ligi ya mabingwa kuliko mchezaji mwingine yeyote
Maelezo ya picha,

Ronaldo amefunga mabao 120 kwenye ligi ya mabingwa kuliko mchezaji mwingine yeyote

Cristiano Ronaldo amesema punde atatangaza mustakabali wake baada ya kuisaidia Real Madrid kushinda kombe mara ya tatu kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa.

Real iliitandika Liverpool 3-1 mjini Kiev siku ya Jumamosi, kutokana na matunda ya GarethBale na shambulio la Karim Benzema

Ingawa Ronaldo hakupachika goli, alimaliza akiwa mfungaji bora msimu huu akiwa na magoli 15.

''siku chache zijazo nitatoa majibu kwa mashabiki'' Ronaldo aliliambia shirika la Bein Sports

''Ilikuwa safi sana kuwa Real Madrid.''Mustakabali wa mchezaji yeyote wa Madrid sio muhimu:muhimu ni kuwa tumeweka historia''.

Alipoulizwa kufafanua kwa nini alitumia sentensi ya wakati uliopita kuhusu kuichezea Madrid,Ronaldo aliongeza, ''Sina shaka, sio muhimu.

''Nahitaji kupumzika, kukutana na timu ya Ureno (Kabla ya Kombe la Dunia) na katika kipindi cha wiki chache ''nitawatangazia ''.

Ronaldo 33 amekuwa na Real Madrid tangu mwaka 2009 na ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2021.

Ni mchezaji wa kwanza kushinda mataji matano ya ligi ya mabingwa tangu kubadilishwa mfumo na kuwa Euefa mwaka 1992.

Lakini alipoulizwa kama hakufurahishwa na kutokufunga goli kwenye fainali, alisema ''Nani hakufurahishwa''? Labda wanapaswa kubadilisha jina la michuano na kuwa michuano ya mabingwa ya CR7, akaulizaa, nani ana mataji mengi? na nani mwenye magoli mengi?''