Zidane:Najivunia kuwa sehemu ya Mafanikio ya Real Madrid

Zinedine Zidane ni Meneja pekee aliyewezesha timu yake kunyakua mataji matatu mfululizo
Maelezo ya picha,

Zinedine Zidane ni Meneja pekee aliyewezesha timu yake kunyakua mataji matatu mfululizo

Zinedine Zidane amesema anajivunia kuweka historia na Real Madrid baada ya kunyakua taji la ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi.

Real Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Gareth Bale akifunga magoli mawili

Real ni timu yenye mafanikio zaidi kwenye historia ya ligi ya mabingwa ikiwa na mataji 13.

Zidane alisema:''hii ni klabu ya wakongwe. Klabu hii imeshinda makombe 13 ya Ulaya nafurahi kuwa sehemu ya historia hii

Aliongeza: '' tunakwenda kufikiria kuhusu tulichokipata, kufurahia wakati huu kwanza.Ni kitu muhimu zaidi kwa sasa''.

Maelezo ya picha,

Real Madrid ilianza na kikosi cha kwanza dhidi ya Liverpool kama walivyofanya kwenye michuano ya mwaka 2016-17

Timu tatu pekee zimeshinda kombe la mabingwa barani Ulaya, Real ikiwa na mataji matano tangu mwaka 1956, Ajax (1971-73) na Bayern Munich (1974-76).

Hata hivyo Real ni ya kwanza tangu kubadilishwa kwa jina la michuano hiyo.

Kiungo Luka Modric anaamini itakuwa ngumu kwa timu kufikia mafanikio ya Real

''Ni jambo la ajabu la kihistoria, aliiambia BT Sport ''Sijui kama kuna mtu atarudia hili siku za usoni.''