Mshambuliaji wa England Raheem Sterling ametetea picha ya tatuu ya bunduki kwenye mguu

Tattoo ya Sterling ilipigwa picha wakati wa mazoezi katika Burton-on-Trent siku ya mapumziko ya Benki Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tattoo ya Sterling ilipigwa picha wakati wa mazoezi katika Burton-on-Trent siku ya mapumziko ya Benki (Bank Holiday Monday)

Mchezji soka wa England Raheem Sterling ametetea tattoo yake mpya ya bunduki kwenye mguu wake akisema ''ina maana kubwa sana" akimaanisha ina uhusiano na mahrehemu baba yake .

Wanaharakati wanaopinga silaha wamemkosoa mshambuliaji huyo wa Manchester City baada ya kuushirikisha umma picha yake ya tattoo ya silaha hiyo aina ya M16 kwenye mguu wake.

Picha hiyo imetajwa kama "isiyokubalika kabisa" na "inayoudhi".

Lakini Sterling amesema ni ishara ya kiapo alichoapa kwamba "hatawahi kushika bunduki" baada ya baba yake kupigwa risasi alipokuwa mvulana mdogo.

Sterling, mwenye umri wa miaka 23, ambaye atakwenda Urusi msimu huu kam sehemu ya kikosi cha England kitakachoshiriki Kombe la Dinia , alifichua tattoo yake kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa anafanya mazoezi na wenzake katika St George's Park.

Haki miliki ya picha @sterling7/Instagram
Image caption Sterling kwa sasa yuko anafanya mazoezi na kikosi cha England kinachojiandaa kwa kombe la Dunia

Lucy Cope, muasisi wa kikundi cha Mama wanaopinga bunduki (Mothers Against Guns) baada ya mwanae kupigwa risasi na kuuawa mwaka 2012, amesema Sterling hapaswi kuichezea England mpaka atakapoondoa tattoo.

Akizungumza na gazeti la Sun alisema: " tatoo hii inaudhi. Raheem anapaswa kuibika. Haikubaliki kabisa.

"Tunadai aondoe ama aifiche tattoo yake na mchoro mwingine .

"Kama atakataa kutusikia basi aondoshwe kwenye timu ya England. Anapaswa kuwa mfano wa kuigwa , lakini badala yake ameamua kuchagua kujipamba na bunduki ."

Sterling, alijiungana timu ya City kutoka Liverpool kwa pauni 49 mwezi wa Julai 2015, alijibu ukosoaji huo kwenye Instagram Jumatatu jioni.

Haki miliki ya picha @sterling7/Instagram
Image caption Mashabiki wengi wa soka waliotoa maoni yao walimtetea Sterling kwenye mitandao ya kijamii

Mchezaji wa zamani wa England ambaye kwa sasa ni mchanganuzi wa masuala ya michezo Gary Lineker amesema kuwa ''Sterling ni mchezaji hatari wa soka mwenye maadili mazuri ya kazi'', na akasema namna gazeti la Sun lilivyomuelezea "inaudhi".

kwa mujibu wa ripoti za awali, baba yake na aliuawa kwa risasi katika mji wa Kingston, Jamaica.

Mada zinazohusiana