Everton kumpa mkataba meneja wa zamani wa Watford Marco Silva

Silva ni miongoni mwa waalimu wanaofundisha soka la kuvutia
Image caption Silva ni miongoni mwa waalimu wanaofundisha soka la kuvutia

Everton ipo karibu kumpa kandarasi meneja wa zamani wa Watford Marco Silva kuiongoza timu hiyo msimu ujao na hilo linaweza kutokea wiki hii.

Silva raia wa Ureno mwenye miaka 40 amekua chaguo la kwanza kwa mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri baada ya kutimuliwa kwa Sam Allardyce mwishoni mwa msimu.

Mkurugenzi mpya wa michezo klabuni hapo Marcel Brands anaanza kazi rasmi siku ya Ijumaa na anataka kupata meneja mpya haraka iwezekanavyo.

Silva anatarajiwa kupewa mkataba wa miaka mitatu ambao unaweza kuongezwa baadhi ya vipengele kutokana na mafanikio atakayoipa Everton.

Silva alitimuliwa Watford mwezi Januari baada ya timu hiyo kufanya vibaya.

Anatajwa kuwa mmoja wa waalimu wanaofundisha soka la kuvutia na anatarajiwa kuleta upinzani mklai kwenye ligi iwapo ataingia Everton.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii