Terry: 'Nimeumizwa sana' Aston Villa kushindwa kucheza ligi kuu

Terry ameondoka Aston Villa baada ya kudumu kwa msimu mmoja
Image caption Terry ameondoka Aston Villa baada ya kudumu kwa msimu mmoja

John Terry amesema ameumizwa sana baada ya Aston Villa kushindwa kufuzu kucheza ligi kuu msimu ujao licha ya kusema kuwa alifanya kila linalowezekana.

Terry nahodha wa zamani wa Chelsea, alijiunga na Villa msimu uliopita na kuchaguliwa kuwa nahodha.

Mchezo wa mwisho kwa Terry mwenye miaka 37 akiwa na Villa ilikua siku ya Jumamosi kuwania kufuzu kucheza ligi kuu ambapo walipoteza mbele ya Fulham.

''Nitaangalia muda nilioutumia hapa na kuona ni namna gani tulikaribia kutimiza malengo yetu,'' alisema Terry.

Image caption Steve Bruce alitegemea kuingoza Villa kwa mara ya tano kucheza ligi kuu

Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza amesema meneja wa Villa Steve Bruce amekua mtu muhimu kwake na amejifunza mengi ambayo hatayasahau maishani.

John Terry kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu

Aliongeza: ''Nilijitoa kwa kila namna kwa mwaka huu ndani na nje ya uwanja, ninaumia sana kuona tumeshindwa kurejea ligi kuu ambapo klabu hii ilipaswa kuwepo kwa asilimia mia moja.''

Terry ambaye amesema klabu ya Villa milele itakuwa moyoni mwake, hajaweka wazi iwapo ataendelea kucheza sehemu nyingine ama la.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii