Kombe la Dunia 2018: Jezi za Nigeria zauzwa zote baada ya watu milioni 3 kuagiza

Alex Iwobi and Wilfried Ndidi Haki miliki ya picha Nike
Image caption Alex Iwobi na Wilfried Ndidi ni miongoni mwa wachezaji wa ligi ya Uingereza waliokuwa wanamitindo wa kuuza nguo hizo mpya

Nigeria huenda sio wanaopigiwa upatu kushinda Kombe la Dunia lakini wanaonekana kupata mashabiki wengi kupitia jezi yao mpya.

Mashabiki milioni 3 tayari wameagiza tisheti kama hizo kulingana na shikisho la soka la Nigeria na wanunuzi walipanga foleni nje ya duka la kampuni ya jezi ya Nike mjini London siku ya Ijumaa ili kujaribu kununua nguo hizo.

Tisheti hizo zilizokuwa zinauzwa kwa bei ya £64.95, ziliuzwa katika tovuti ya kampuni ya Nike muda mfupi baada ya kutolewa.

Kiungo wa kati wa Arsenal Alex Iwobi ni miongoni mwa waliouza jezi hizo ambazo zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Februari , pamoja na mchezaji wa Leicester Wilfried Ndidi, ambaye alivaa kofia na jaketi katika picha za kampeni ya kuziuza jezi hizo.

Nigeria inatarajiwa kuvaa jezi hizo mpya wakati itakapokabiliana na Uingereza katika mechi ya kirafiki ya kombe la dunia katika uwanja wa Wembley Jumamosi Usiku.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Wapita njia wakisambaziana picha za foleni nje ya duka la Nike mjini London
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mtangazaji wa BBC Radio 1Extra Dotty ni shabiki mpya wa Nigeria
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Baadhi ya mashabiki walikuwa na njia tofauti za kunua tisheti hizo