Yaya Toure: 'Guardiola alinionyesha ukatili, alinichukulia adui na alinionea wivu'

Yaya Toure (kushoto) alianzishwa mechi moja pekee ya ligi msimu wa 2017-2018 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Yaya Toure (kushoto) alianzishwa mechi moja pekee ya ligi msimu wa 2017-2018

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ana matatizo na Waafrika , kulingana na aliyekuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Yaya Toure.

Raia huyo wa Ivory Coast ambaye aliondoka City mwezi Mei baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka minane katika klabu hiyo anasema kuwa anataka kuvunja mtazamo wa Guardiola ambaye amemtaja kuwa mwenye wivu.

''Pengine sisi Waafrika hatuchukuliwi kama wengine wanavyochukuliwa'', alisema Toure katika mahojiano na soka ya Ufaransa.

Klabu ya Uingereza ya Man City imekataa kuzungumzia kuhusu matamshi ya Toure.

Kabla ya kuondoka , klabu hiyo iliutaja uwanja mmoja wa mazoezi jina lake na baadaye kuzindua picha yake katika uwanja huo.

Msimu ujao Manchester City inatarajiwa kumsajili raia wa Algeria Riyad Mahrez kutoka Leicester City.

Image caption Yaya Toure: Guardiola alinionyesha ukatili, alinichukulia adui na alinionea wivu

Toure, ambaye ni raia wa Ivory Coast alicheza katika klabu ya Barcelona kwa misimu miwili chini ya usimamizi wa Guardiola kabla ya kuuzwa kwa klabu ya City kwa dau la £24m 2010.

Alijishindia mataji sita nchini Uingereza lakini akaanzishwa mechi moja pekee katika msimu wake wa mwisho katika klabu hiyo ambapo City ilishinda taji la ligi katika mechi ya mwisho dhidi ya Brighton.

Kabla ya mechi hiyo, Guardiola alisema: Yaya alikuja hapa mwanzo wa safari. Tulipofikia hivi sasa ni kutokana na juhudi zake. Mechi ya Brighton ni mechi ambayo tutampatia ikiwa mojawapo ya maagano mazuri ambayo mchezaji angefaa kupatiwa.

Toure alicheza dakika 86 dhidi ya Brighton , baada ya kucheza dakika 142 pekee katika msimu wote. Anaamini kwamba sababu ya yeye kutochezeshwa sio umri wake wala maungo yake, akisema kuwa alitafuta data kutoka kwa maafisa wa mazoezi ili kujilinganisha na wachezaji wenye umri mdogo.

Guardiola alishinda mataji sita kama mchezaji wa Barcelona na ameongeza mataji mengine saba kama mkufunzi akisimamia klabu hiyo ya Catalan, Bayern Munich na City.

Toure alisema: Sijui kwa nini nina hisi kwamba alikuwa na wivu, alinichukulia kama adui. Kama ambaye nilimuonyesha kuwa mtu mdogo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yaya Toure adai Guardiola alimuonyesha ukatili

Alinionyesha ukatili , nilijiuliza iwapo ni kwa sababu ya rangi yangu. Mimi sio wa kwanza kuzungumza kuhusu tofauti ya tunavyochukuliwa .

Katika klabu ya Barca kuna wengine wameuliza swali kama hilo. Tunapogundua kwamba ana matatizo na wachezaji wa Afrika kila anapokwenda , najiuliza maswali mengi. Nataka kuwa mchezaji ambaye nitavunja mtazamo wa Guardiola.

Toure alianzishwa mechi 22 pekee chini ya usimamizi wa Guardiola msimu wa 2016-17 na akaambiwa asalie katika klabu hiyo kwa mwaka mwengine mmoja, lakini akatumiwa kidogo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii