Forbes: Floyd Mayweather ndio mwanamichezo tajiri zaidi duniani

Floyd Mayweather v Conor McGregor Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mayweather (kushoto) na McGregor walizipiga katika pigano lao la raudni 10 mwezi Agosti 2017

Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika porodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.

Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ua masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.

La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa.

Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema

Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12.

Mayweatjher ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m

"Mechi kubwa kati yake na McGregor 2017 iliwasaidia Mayweather na McGregor kujipatia pato la jumla ya $400m'' , alisema Kurt Badenhausen, Mhariri mkuu wa jarida wa Forbes Media.

"Lakini wachezaji wa mpira wa vikapu wametawala orodha ya wanamichezo 100 kufuatia kuongezwa kwa mishahara yao inayotokana na kandarasi ya maouyesho ya runinga ya $24bn

Aliongezea: "Orodha ya Forbes' ya wachezaji wanaopata mapato ya juu imejaa wanaume. lakini kumekuwa na mchezaji mmoja wa kike ambaye alifuzu baada ya orodha hiyo kuongezwa hadi majina 50 2010.

Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.

  1. Floyd Mayweather - Ndondi ($285m)
  2. Lionel Messi - Kandanda ($111m)
  3. Cristiano Ronaldo -kandanda($108m)
  4. Conor McGregor - Karate, judo na Ndondi ($99m)
  5. Neymar - kandanda ($90m)
  6. LeBron James - Vikapu ($85,5m)
  7. Roger Federer - tenisi ($77.2m)
  8. Stephen Curry - Vikapu ($76.9m)
  9. Matt Ryan - Soka ya Marekani ($67.3m)
  10. Matthew Stafford - Soka ya Marekani ($59.5m)

Tazama Orodha kamili

Marekani yatawala

Floyd Mayweather, Cristiano Ronaldo na Tiger Woods - wakiwa katika nambari 16 mwaka huu ndio wanamichezo watatu waliopo katika orodha ya wanamichezo tajiri zaidi ambao wamesalia katika orodha hiyo katika kipindi cha miaka 18 iliopita.

Mapato ya 2018 yalikuwa $22.9m, juu kutoka 1.5m mwaka uliopita kutokana na nyongeza ya mishahara miomgoni mwa wachezaji wa NBA.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lewis Hamilton ndio mwanamichezo wa Uingereza aliye na mapato ya juu

Wanamichezo 11 kutoka michezo tofauti wameorodheshwa katika orodha hiyo na kutoka mataifa 22

Nyota wa ligi ya vikapu ya NBA wanaongoza katika orodha hiyo wakiwa wachezaji 40 miongoni mwa 100 tajiri.

Soka ya Marekani ndio mchezo wa pili uliowasilishwa sana ukiwa na wachezaji 18 , na kufuatiwa na mchezo wa baseball ukiwa na wachezaji 14 huku kandanda ikiwasilishwa na wachezaji 9 pekee.

Marekani ilitawala orodha hiyo ikiwa na wanariadha 66 huku Uingereza ikiwa na 5 wanaoongozwa na dereva wa F1 Lewis Hamilton katika nambari ya 12 na mapato ya $51m.

Mataifa ya Dominican na Uhispania yana wanariadha 3, hukiu Argentina, Brazil, Ufaransa, Japan na Venezuela wakiwa na wawili wawili.