Tetesi za soka Ulaya Jumatano 06.06.2018

Aliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc
Image caption Aliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc

Chelsea inakaribia kumsajili aliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc kuchukua mahala pake Antonio Conte. (Express)

Manchester United wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili beki wa Sevilla Clement Lenglet, 22.

Haki miliki ya picha Getty Images

Raia huyo wa Ufaransa ana kifungu cha kandarasi yake kitakachogharimu £30.7m ili kuondoka katika klabu hiyo. (L'Equipe - in French)

Liverpool inapanga dau la £10m kumnunua winga wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 Moses Simon kutoka klabu ya Gent. (Liverpool Echo)

Image caption Liverpool inapanga dau la £10m kumnunua winga wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 Moses Simon kutoka klabu ya Gent. (Liverpool Echo)

Leicester inaongoza katika kumsajili kiungo wa kati wa Norwich James Maddison, 21, huku klabu hiyo ikitaka kupewa zaidi ya £20m ili kumuuza raia huyo wa Uingereza. (PA)

Leicester imeanzisha mazungumzo ya kutaka kumsaini beki wa Ireland kaskazini Jonny Evans, 30, ambaye anapatikana kwa dau la £3m baada ya kushushwa daraja na klabu ya West Brom. (Mirror)

West Brom imekataa ombi la £4m kutoka kwa klabu ya Stoke kumsaini winga wa Ireland Kaskazini James McClean, 29. (Birmingham Mail)

Chelsea, Tottenham na West Ham wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon, 28, ambaye anapatikana kwa kitita cha £16m. (Mirror)

Image caption Chelsea, Tottenham na West Ham wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon, 28,

Wolves imeanza mazungumzo ya kutaka kumsaini beki wa kulia wa Valencia Joao Cancelo, 24, na dau la £35m tayari linajadiliwa kumchukua raia huyo wa Ureno. (Sky Sports)

Mkurugenzi mpya wa kandanda Marcel Brands anasema kuwa klabu hiyo itajaribu kuwauza hadi wachezaji 12 msimu huu (Mirror)

Watford itakataa na winga wake mwenye thamani ya £40m- Richarlison iwapo mkufunzi mpya wa Everton Marco Silva atamuhitaji mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa 21. (Evening Standard)

Mada zinazohusiana