Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 07.06.2018

Jorginho Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester City huenda wakakubali mkataba wa thamani ya pauni milioni 43 kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho, mwenye umri wa miaka 26, kufikia mwishoni mwa wiki, huku ajenti wamechzaji huyo wa kimataifa akiwa ameelekea England. (Mirror)

City huenda wakamuwania mchezaji wakiungo cha kati wa Southampton raia wa Gabon Mario Lemina au mchezaji wa Real Madrid Mateo Kovacic, wote walio na umri wa miaka 24, iwapo timu hiyo haitofanikiwa kumsajili Jorginho. (Mail)

Wawakilioshi wa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Liverpool Mohamed Salah wamekana kumuuza raia huyo wa Misri mwenye umri wa miaka 25 kwa Barcelona. (Ramy Abbas Issa on Twitter)

Real Madrid itamlenga meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya hatua ya kushtusha ya kujiuzulu kwa Zinedine Zidanewiki iliopita. (Mail)

Liverpool wanajitayarisha kumsaka winga wa Stoke raia wa Usiwzi Xherdan Shaqiri, mwenye umri wa miaka 26, ambaye mkataba wake unahitaji alipiwe pauni milioni 12 ili aruhusiwe kuihama klabu hiyo. (star)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapigiwa upatu kuvuka Real Madrid

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Liverpool Roberto Firmino anasema kipa wa Roma Alisson, mwenye umri wa miaka 25, amemuuliza kuhusu uwezekano wa kuhamia Anfield msimu huu wa joto. (Liverpool Echo)

Liverpool wametakiwa watoe £ milioni 80 na Atletico Madrid iwapo wanataka wamsajili kipa raia wa Sloveni Jan Oblak msimu huu wa joto. (Mirror)

Manchester United, Chelsea na Paris St-Germain wamepewa nafasi y kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski lakini Bayern Munich haitomuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa kiwango kilicho chini ya £ milioni 175. (Bild - in German)

Arsenal imependekezewa ombi la thamani ya £ milioni 26 kwa mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Ureno Gelson Martins,aliyekataliwa na Sporting Lisbon. (A Bola - in Portuguese)

Tottenham itashindana na Chelsea kumsajili mlingi wa England Jamaal Lascelles, ambaye thamani yake inatajwa kuwa £milioni 45 na Newcastle. (Evening Standard)

Arsenal inakaribia kumsajili mchezaji chipukizi wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 17 wa kiungo cha kati Yacine Adli kutoka Paris St‑Germain. (Guardian)

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Newcastle ina hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa Jack Grealish (kulia)

Newcastle ina hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 22, lakini timu hiyo ya mabingwa inataka £ milioni 40 kwa mchezaji huyo wa England. (Chronicle)

Southampton inafikiria kumwania Keinan Davis, wa Aston Villa na winga Andre Green. (Mail)

Winga wa Watford Roberto Pereyra, amehusishwa na uhamisho kwenda Torino, ambako atajiunga na aliyekuwa mkuu wa Hornets Walter Mazzarri. (Harrow Times)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Derby Frank Lampard ataka kumsajili mchezaji wa Chelsea John Terry

Meneja wa Derby Frank Lampard atamsajili mchezaji wa Chelsea John Terry, mwenye umri wa miaka 37, katika uhamisho wa bure iwapo kampteni wa Rams Curtis Davies, mwenye umri wa miaka 33, ataondoka. (Mirror)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard anakaribia kukubali mktaba wa mkopo wa msimu mzima kwa mchezaji wa Liverpool Ovie Ejaria, mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)

Timu iliyopandishwa daraja hivi karibuni katika Serie A - Parma inajitayarisha kumwania aliyekuwa mshambuliaji wa England Peter Crouch, mwenye umri wa miaka 37. (Calciomercato via Talksport)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii