Simba kukutana na Gor Mahia fainali Kombe la SportPesa

Kegere amefunga mabao yote mawili ya Gor Mahia dhidi ya Singida FC

Chanzo cha picha, SportPESA

Maelezo ya picha,

Kegere amefunga mabao yote mawili ya Gor Mahia dhidi ya Singida FC

Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya kuwacharaza Kakamega Homeboyz wa Kenya kwa mikwaju 5-4 ya penalti.

Watakutana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia ambao wameibuka washindi kwa kuwanyuka Singida FC wa Kenya 2-0.

Mabao hayo yamefungwa na Meddie Kagere.

Mechi za nusu fainali zilichezewa uwanja wa Afraha, Nakuru.

Simba walifika nusu fainali baada ya kuwaondoa Kariobangi Sharks wa Kenya.

Singida FC walifika nusu fainali kwa kuwaondoa mahasimu wa jadi wa Gor Mahia AFC Leopards.

Chanzo cha picha, SPORTPESA

Maelezo ya picha,

Mvua kubwa ilinyesha wakati wa mechi kati ya Gor Mahia na Singida

Chanzo cha picha, SPORTPESA

Kakamega Homeboyz ndio waliokuwa wamewatoa mashindanoni timu kongwe nchini Tanzania Yanga kwa kuipachika mabao 3-1 kwenye mechi ya ufunguzi.

Jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo.

Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.

Chanzo cha picha, SPORTPESA

Maelezo ya picha,

Mashabiki wa Simba uwanjani

Chanzo cha picha, SPORTPESA

Maelezo ya picha,

Shabiki wa Kakamega Homeboyz

Bingwa mtetezi Gor Mahia ndiyo iliyocheza na Everton mwaka jana jijini Dar es Salaam ikapoteza kwa mabao 2-1, wafungaji wa Everton wakiwa ni mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney na Kieran Dowell, naye Jacques Tuyisenge akaipa Gor Mahia bao lao moja.