Maafisa wa soka akiwemo Mkenya wanaswa wakipokea fedha

Maafisa wa soka akiwemo Mkenya wanaswa wakipokea fedha

Maafisa 100 wa soka Magharibi mwa Afrika na Kenya wamenaswa na kamera za siri za mwandishi wa habari za uchunguzi na upekuzi wa Ghana, wakipokea rushwa.

Hatua hii ni sehemu ya uchunguzi wa miaka miwili uliofanywa na mwandishi huyo Anas Aremeyaw.

Miongoni mwa wanaotuhumiwa ni pamoja na refa mmoja kutoka Kenya Aden Range Marwa, ambaye alitarajiwa kusimamia mechi za kombe la dunia nchini Urussi na Kwesi Nyantekyi, Rais wa shirikisho la soka nchini Ghana ambaye pia ni mwanachama wa baraza kuu la shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.

Marwa amekanusha madai hayo naye Nyatekyi hajasema lolote.

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Ghana limesema, litachunguza madai hayo kutokana na uzito wake.