Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 08.06.2018

Alikyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Real Madrid fernando Hierro

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aliyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Real Madrid fernando Hierro

Aliyekuwa beki wa Real Madrid Fernando Hierro ameorodheshwa katika orodha ya wakufunzi wanaotarajiwa kumrithi aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane katika klabu hiyo(AS)

Mabingwa wa ligi ya La Liga Barcelona na Real Madrid wanashindana katika kutaka kumsajili winga kinda wa klabu ya Santos Rodrygo Goes, 17. Raia huyo wa Brazil anaweza kuondoka katika klabu hiyo iwapo wananuzi watalipa dau la £44m (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham itaiweka klabu ya Aston Villa katika majaribu kupitia ombi la kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish 22 ambaye ana thamani ya £40m. (Telegraph)

Tottenham itasitisha hamu yao ya kumsaka winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 25, baada ya kutakiwa kutoa kitita cha £70m ili kumsajili winga huyo wa Ivory Coast. (Mail)

Majadiliano kati ya Manchester United na Tottenham hotspurs kuhusu mchezaji Toby Alderweireld, 29, yamegonga mwamba baada ya Spurs kuitisha zaidi ya dau la £55m kumsajili beki huyo wa Ubelgiji.. (Evening Standard)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho huenda asifanye usajili wa beki wa kushoto msimu ujao na badala yake huenda akatumia fedha hizo kutafuta mchezaji anayeweza kumsaidia mshambuliaji wakew Romelu Lukaku msimu ujao. (Independent)

Manchester United na klabu mbili za ligi ya China zimewasilisha dau la £35m kumsajili kiungo wa kati wa Benfica na Brazil Anderson Talisca ,24, ambaye Lazio inasema ana thamani ya £44m, . (O Jogo - in Portuguese)

West Ham iko katika mazungumzo kumsaini kiungo wa kati wa Brazil Felipe Anderson, 25, ambaye ana thamani ya £44m by Lazio. (Sky Sports)

West Ham imeanza mazungumzo ya kutaka kumsaini aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester City Kolo Toure 35, kwa uhamisho wa bure. (Mail)

The Hammers wanasema kuwa mshambuliaji wake Marko Arnautovic ,29, ana thamani ya £60m huku Manchester United ikidaiwa kumnyatia raia huyo wa Austria. (Mirror)

Chanzo cha picha, Reuters

Liverpool inataka kumsaini kipa wa Bayer Leverkusen Bernd Leno, 26, lakini italazimika kulipa £22m ili kumsajili raia huyo wa Ujerumani. (Bild - in German)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anataka kuunganishwa tena na beki wa zamani wa timu ya Liverpool Martin Skrtel. Raia huyo wa Slovakia 33, yuko huru kuondoka klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (Aspor - in Turkish)