Fred anayetarajiwa kujiunga na Man United apata jeraha katika mazoezi

Fred alijeruhiwa wakati wa mazoezi ya timu ya Brazil mjini London Uingereza

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Fred alijeruhiwa wakati wa mazoezi ya timu ya Brazil mjini London Uingereza

Kiungo wa kati wa Brazil Fred, anayetarajiwa kujiunga na klabu ya Manchester United amepata jeraha katika kifundo chake cha mguu katika mazoezi kabla ya kuanza kwa kombe la dunia.

United wamekubaliana dau la £47m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk huku uhamisho huo ukitarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Maelezo ya video,

Maafisa wa soka akiwemo Mkenya wanaswa wakipokea fedha

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Fred alipata jeraha kutokana na makabiliano na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro

Daktari wa timu ya Brazil Rodrigo Lasmar alilitaja jeraha hilo lililotokea mjini London kuwa lenye maumivu makali katika mguu wake.

Brazil inaanza kampeni yake ya kombe la dunia dhidi ya Switzerland tarehe 17 mwezi Juni.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Alionekana kuwa na uchungu baada ya kifundo chake cha mguu wa kulia kufungwa bandeji

Washindi hao mara tano wa kombe la dunia baadaye watacheza katika kundi E dhidi ya Costa Rica na Serbia nchini Urusi.

Lasmar aliongezea: kwa sasa ni mapema mno kusema chochote kuhusu hali yake. Siku ya Ijumaa tutaangalia tujue kitakachofanyikana kuamua iwapo tunahitaji kufanya uchunguzi wowote ama la.