Gor Mahia ya Kenya, Simba ya Tanzania kivumbi hii leo kombe la SportPesa

Mashabiki wa Gormahia wakifuatilia mchezo uwanjani
Image caption Mashabiki wa Gormahia wakifuatilia mchezo uwanjani

Michuano ya SportPesa Super Cup 2018 inatarajiwa kukamilika leo kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji, Gor Mahia ya Kenya na Simba SC ya Tanzania Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya.

Simba SC imefika Fainali baada ya kuzitoa Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys za Kenya zote kwa penalti baada ya sare ya 0-0.

Gor Mahia ilizichapa 3-0 JKU ya Zanzibar na 2-0 Singida United ya Tanzania.

Image caption Mashabiki wa timu ya Simba Sc

Bingwa wa SportPesa Super Cup mwaka 2018, atapata dola za Kimarekani 30,000 pamoja na nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England.

Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.

Gor Mahia ndiye bingwa mtetezi ambaye mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mada zinazohusiana