Afrika yataka uandalizi wa kombe la dunia kuzunguka

Afrika kusini ndio taifa la pekee kuandaa kombe hilo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Afrika kusini ndio taifa la pekee kuandaa kombe hilo

Marais wa Mashirikisho ya soka barani Afrika wameitaka Fifa kurudisha mfumo wa mzunguko ili kuliwezesha kila bara kuandaa awamu moja ya michuano ya kombe la dunia.

Hii ni baada ya Morocco kupoteza dhidi ya Marekani kwa kura 134 kwa 65 kwenye kinyanganyiro cha kumsaka mwandalizi wa kombe la dunia mwaka 2026.

"Njia ya mzunguko itakuwa suluhisho bora," amesema rais wa mpira Malawi, Walter Nyamilandu.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Kiongozi wa shirikisho la soka Liberia Musa Bility

"Tunafaa kutoa ombi la kukarabatiwa njia za kumsaka muandaaji wa kuombe la dunia ili kuwezesha kurudhishwa kwa mtindo wa bara moja kuliandaa kombe,".

Bility ambaye pia ni mwanachama wa bodi ya makatibu wa shirilisho la soka barani CAF, ameitaka FIFA kuangazia njia hiyo akiitaja kuwa Kombe la dunia ni kufikisha soka kwa wapenzi wake.

Njia hiyo iliyoanzishwa mwaka wa 2001 kabla ya kutupiliwa mbali 2007, imekuwa na manufaa kwa Afrika kwani mwaka wa 2010 Afrika iliandaa dimba la dunia lililofanyika nchini Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bility

Rais wa zamani wa Fifa Sepp Blatter alileta pendekezo hilo baada ya taifa ya Afrika Kusini kupoteza kura za kuwa mwandalizi mwaka wa 2006.

Pigo la Morocco dhidi ya Canada, Mexico na Marekani linamaanisha kuwa bara la Afrika limeandaa kombe la dunia mara moja kati ya Makala ishirini na tatu ilihali Mexico pekee imeanda kombe mara tatu.

Ingawa Liberia ni mojawapo ya mataifa yaliyoipa kisogo Morocco, Rais Bility analaumu ukosefu wa njia ya kuyasawazisha mataifa yote.

'Mataifa yote duniani hayako sawa kwa hivyo sheria za kuwezesha shindano kuandaliwa maeneo tofauti zinahitajika, hakuna namna Moroco ingeibwaga Marekani,'' alisema Bility.

Matokeo ya kura za kumsaka mwandalizi wa Kombe la dunia yamewaacha wengi vuinywa wazi wajumbe wakiuliza maswali ya ni lini Afrika litaandaa tena Kombe jhilo.