Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 14.06.2018

Jack Grealish

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jack Grealish

Tottenham wameipa Aston Villa ofa ya pauni milioni 15 kwa kiungo wake wa kati Jack Grealish, lakini Chelsea, Fulham na Leicester pia wanamtaka mchezaji huyo wa maiaka 22. (Sky Sports)

Burnley wanataka kuwasaini mlinzi wa England Craig Dawson, 28, na mshambuliaji wa England Jay Rodriguez, 28, kutoka West Brom kwa pauni milioni 28 kwa pamoja. (Mail)

Arsenal wako kwenye mazungumzo na Bayern Leverkusen kumsaini kipa mjerumani Bernd Leno, 26. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lucas Torreira

Arsenal wanakaribia kutumia pauni milioni 50 kununua wachezaji wakiwemo kiungo wa kati wa Sampdoria raia wa Uruguay Lucas Torreira, 22, na beki wa Borussia Dortmund mgiriki Sokratis Papastathopoulos, 30. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Manchester City Mhispania Brahim Diaz, 18, anatafutwa na meneja wa West Ham Manuel Pellegrini kwa mkopo wa muda mrefu. (Sun)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jerome Boaten

Mlinzi wa Ujerumani Jerome Boateng, 29, ambaye anawinda na Manchester United, ataruhusiwa kuondoka Beyern Munich kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa klabu, Karl-Heinz Rummenigge. (Manchester Evening News)

Mlinzi wa Newcastle raia wa Congo Chancel Mbemba, 23, amekubali mkataba wa miaka minne na Porto wa thamani ya pauni milioni 8. (Mirror)

Meneja wa Derby Frank Lampard anamtaka mchezaji wa Chelsea wa miaka 20 raia wa England Jay Dasilva. (Talksport)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Sadio Mane

Mshambuliji wa Liverpool Sadio Mane, 26, anasisitiza kuwa yuko na furaha huko Liverpool baada ya uvumi kuwa anataka kuhamia Real Madrid. (BT Sport)

Kocha wa Jeventus Massimiliano Allegri, 50, anasema alizungumziwa na Real Madrid kuhusu kuchukua mahala pake Zinedine Zidane - lakini akakataa. (The Sun)

Kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Yacine Adli, 17, huenda akakataa kujiunga na Arsenal ili kusalia kwenye klabu hiyo ya Ligue 1. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Antoine Griezmann

Real Madrid watahitajika kuipa Roma pauni miloni 52.83 ili kumpata kipa raia wa Brazil Alisson, 25. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid mfaransa Antoine Griezmann atafichua mipango yake ya siku za usoni leo Alhamisi - mchezaji huyo wa miaka 27 amehusishwa na kuhamia Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich atahitaji kufanya uamuzi mgumu wa kufanya ikiwa atamfuta Antonio Conte nakumlipa hadi pauni milioni 9 kama fidia au amruhusu raia huyo wa Italia kumaliza mwaka wake wa mwisho. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Antonio Conte