Ratiba Ligi Kuu England 2018-19: Man City kukutana na Arsenal siku ya kwanza

Manchester City celebrate

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester City wakisherehekea kushinda taji la Ligi ya Premia 2017-18

Mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City wataanza msimu kwa mechi ya ugenini dhidi ya Arsenal wikendi ya 11-12 Agosti msimu mpya wa Ligi Kuu England utakapoanza.

Arsenal wataanza msimu wakiwa na meneja mpya Unai Emery aliyemrithi Arsene Wenger, Mfaransa aliyeondoka klabu hiyo baada ya kuwa kwenye usukani kwa miaka 22.

Tottenham watasafiri Newcastle kisha wacheze dhidi ya Fulham katika uwanja wa Wembley wakisubiri uwanja wao mpya unaogharimu £850m umalize kujengwa.

Manchester United watakuwa wenyeji wa Leicester City, Liverpool nao wakutane na West Ham, huku mabingwa wa Championship Wolverhampton Wanderers wakialika Everton uwanja wao wa Molineux.

Fulham waliopandishwa daraja watakuwa wenyeji wa Crystal Palace, huku Cardiff wakiwazuru Bournemouth.

Chelsea watasafriHuddersfield, Southampton wawe wenyeji wa Burnley, nao Watford wakabiliane na Brighton uwanjani Vicarage Road.

Mechi za wikendi ya kwanza

Mechi zitakazofuata:

JUMAMOSI 18 AGOSTI

 • Brighton & Hove Albion v Manchester United
 • Burnley v Watford
 • Cardiff City v Newcastle United
 • Chelsea v Arsenal
 • Crystal Palace v Liverpool
 • Everton v Southampton
 • Leicester City v Wolverhampton Wanderers
 • Manchester City v Huddersfield Town
 • Tottenham Hotspur v Fulham
 • West Ham United v AFC Bournemouth

JUMAMOSI 25 AGOSTI

 • Arsenal v West Ham United
 • AFC Bournemouth v Everton
 • Fulham v Burnley
 • Huddersfield Town v Cardiff City
 • Liverpool v Brighton & Hove Albion
 • Manchester United v Tottenham Hotspur
 • Newcastle United v Chelsea
 • Southampton v Leicester City
 • Watford v Crystal Palace
 • Wolverhampton Wanderers v Manchester City