Mapenzi, mabao na kuwang'ata watu - kuibuka kwa Luis Suarez

Luis Suarez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luis Suarez

Luis Suarez sasa mwenye miaka 31 ameshinda ligi ya klabu bingwa barani Ulaya, akashinda vikombe kadhaa vya La Liga na Barcelona, akashinda kiatu cha dhahabu cha mchezaji cha mwaka katika Ligi ya Premia na mchezaji wa mwaka akiwa na Liverpool na ndiye mfungaji bora zaidi wa Uruguay.

Lakini ndoto yake ya kucheza mpira ilianza wakati alikopa viatu huko Mantevideo na pia ndoto yake ya kutaka kujiunga na mpenzi wake Sofia wakati familia ya mpenzi huyo wake ilihamia Barcelona Suarez akiwa na miaka 16.

Kutokana na kujiunga na klabu ya Urreta kama kijana wa miaka saba na kuwa mchezaji aliyetafutwa sana huko Ajax, BBC inafuatilia safari ya Suarez kutoka kwa wale waliomfahamu vyema.

Alikopa viatu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luis Suarez ndiye mfungaji bora Uruguay

Suarez alizaliwa huko Salto Januari mwaka 1987, akahamia Montevideo akiwa na umri wa miaka 7 na wazazi wake pamoja na ndugu zake 6. Hapa ndipo alianza kucheza kandanda ya watoto katika klabu ya Urreta.

Pablo Parodi, rafiki na jirani wa familia ya Suarez huko Montevideo: "Alikuwa mtoto mtulivu hakuwa mtoto ambaye angetambuliwa. Wakati mwingine alikuwa akishinda na ndugu zake, alikuwa mtulivu na mwenye heshima".

"Wakati mwingine alikuwa anakuja kwenye duka la mikate ale keki au kitu kitamu, ili asienda kugawana na ndugu zake kwa sababu walikuwa wengi.

Wilson Piris, ajenti wa kwanza wa Suarez: "Ndugu zake, familia yake yote, walikuwa watu wenye nidhamu. Nafikiri aliiga hilo nyumbani.

"Akiwa na miaka 12, Luis alikuwa na nia ya kusaidia nyumbani kwa njia ambayo angesaidia wakati huo. Na wakati wa wikendi angepata pesa kutoka kwetu kwa kufunga mabao.

Ndoto ya Barcelona

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez alitimiza ndoto ya kujiunga na Barcelona

Uwezo wa kijana huyo ulivutia moja ya klabu kubwa zaidi nchini Uruguay, Nacional na akajiunga na klabu ya vijana ya huko Montevideo akiwa na miaka 14.

Di Candia: "Luis alikuwa tayari amejitambulisha kama mfungaji mabao. Wakati mechi ingekamilika kwa mabao 5-0, 8-0, 8-2, angeweza kufunga mabao manne au matano. Kwa hivyo dalili zilianza kuonekana mapema kuwa angekuja kuwa mchezaji mzuri.

Alikuwa na nguvu sana na mwenye hasira wakati ule sawa na sasa. Luis angegombana na wachezaji wenzake ikiwa hawangempa mpira, kuhusu penalti na kadhalika, Alikuwa mwenye hasira sana.

Piris: "Kuna baadhi yetu ambao walimuamini sana Luis, kwa sababu alikuwa na tabia fulani na mbinu ya kucheza. Alikuwa ni mtoto ambaye angepata mpira wakati watoto wengine wangekosa na kufunga.

"Nilishuku angefanikiwa na kuwa mchezaji mzuri siku za usoni kwa sababu alisema angeichezea Barcelona.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luis Suarez

'Suarez alikuwa na safari ndefu'

Suarez alijunga na kikosi cha kwanza cha timu, akiwa na miaka 18 na kufunga mara kumi kwenye mechi 27 wakati Nacional ilishinda ligi ya Uruguay.

Martin Lasarte, ambaye alimwezesha Suarez kujiunga na Nacional: "Mara ya kwanza nilimuona Suarez ni wakati alikuwa anawasili uwanjani kufanya mazoezi. Yalikuwa mazoezi mara mbili, alikuwa amekosa ya asubuhi kwa sababu alikuwa amesafiri kutoka Uhispania na alikuwa ameshinda kwa nyumba ya mpenzi wake.

"Tulielewa kwa haraka kuwa atakuwa mtu tofauti. Alikuwa na uwezo ambao sikuwa nimeuona kwa wachezaji wakubwa. Alikuwa na vitu ambavyo bado alistahili kuvifanya, alikuwa ni kama almasi ambayo haikuwa imesafishwa lakini uwezo wake ulikuwa mkubwa kuliko ya mtoto wa umri wake.

"Kawaida angezungumzia ndoto zake wakati tukifanya mazoezi uwanjani, alisema angeichezea Barcelona. Akiwa na miaka 18, nilifikiri "mtoto huyo ana safari ndefu lakini baadaye alifanikiwa."

Suarez alihama kwa sababu ya mapenzi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rons Jans (kulia) alikuwa meneja wa Groningen wakati walisaini Suarez kutoka Nacional

Mwaka 2006 Groningen ilituma maajenti kwenda Uruguay kumtafuta mchezaji wa kumsaini- walirudi na Luis Suarez baada ya kijana huyo kuwafurahisha maajenti hao kutoka Uholanzi. Lakini sio mpira tu uliokuwa akilini mwa Suarez kutaka kuhamia Ulaya...

Lasarte: "Alianza kuniambia kuhusu mpenzi wake na umbali uliopo , kikiwa ndicho kitu tu kimewatenganisha kwa sababu walikuwa wanapendana sana. Hadithi ya mapenzi ilikuwa na nguvu kifyake. Ilikuwa muhimu zaidi kuliko hata kufanikiwa katika kandanda.

"Kila mara angesema yuko mbali sana, alikuwa amemkosa sana au kila mmoja alikuwa anamkosa mwingine. Kama kungekuwa na fursa ya kuonana wangefanya hivyo.

Mario Rebollo, aliyekuwa wa kwanza kutambua kipaji cha Suarez akichezea timu ya vijana wa chini ya miaka 15 ya Nacional yeye alipokuwa kocha wa Montevideo Wanderers anasema Suarez alifanya kila aliloweza kuhakikisha anakuwa karibu na mpenzi wake Sofia aliyekuwa anaishi Barcelona.

"Luis alikuwa anapendana sana na Sofia na mpaka wa leo hunilalamikia kwamba tulimlazimisha kufika kwenye klabu kwa mazoezi ya kuanza kwa msimu, na kufikisha kikomo likizo yake na mpenzi wake, na kwamba baadaye hatukumchagua moja kwa moja awe kwenye kikosi cha timu ya kwanza."

Uzani wa juu wa mwili

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez akiwa na Uruguay

Baada ya kumnunua kwa pauni 720,000, Groningen ilimruhusu Suarez muda zaidi kupumzika baada ya mkataba wake na Nacional kukamilika. Aliwasili akiwa ameongeza uzani lakini aliye tayari kujifunza kiholanzi na kujumuika nao.

Jans: Alifika akiwa amechelewa. Ilikuwa vizuri kwa sababu mwili na akili vinahitaji kupumzika. Lakini aliwasili akiwa ameongeza uzani. Kwa hivyo nilimuambia hakua katika kikosi cha kwanza. Alifanya mazoezi mara moja na hakuyapenda.

Nikamwambia: Kama utafanya mazoezi kwa njia hii, hauwezi kuingia kwenye kikosi cha kwanza, kama hauwezi kupunguza uzani huwezi kucheza. Wajibu wa kwanza ulikuwa ni kupoteza kilo mbili kabla nifikiri kumweka katika kikosi cha kwanza. Ilisaidia sana katika uhusiano wetu lakini pia ilimpa motisha ya kufanya vizuri.

Suarez akaanza kufanikiwa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez alifunga ara mbili twakati s Groningen iliishinda Vitesse 3-1

Suarez alijisukuma na akamaliza msimu kwa magoli 10 katika mechi 29 za ligi yakiwemo mabao mawili kwenye dakika 10 za mwisho wakati wa ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Vitesse. Kutokana na umaarufu alioupata Ajax wakaanza kumwinda.

Jans: "Wakati wa mechi kabla ya ile yaVitesse nilifanya mabadiliko na kumtoa. Hakufurahishwa na hilo, sikufurahishwa na jinsi aliitikia. Lakini baada ya hili tulishangilia na umati wote na ilikuwa vizuri.

"Kwangu kitu kilichokuwa kikuu ni aanze katika kikosi cha kwanza. Kimwili alihitaji muda zaidi, lakini alikuja kujulikana kama mshambuliaji wa kipekee.

"Alikuwa na furaha hapa. Aligundua kuwa alikuwa anafanya viema na wakati unapongezwa na wachezaji wenzako unapata kujiamini ziadi.

Kuelekea Amsterdam

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez alifunga mabao 22 msimu wa kwanza huko Ajax

Suarez akasaini mkataba wa pauni milioni 6.75 na Ajax Agosti mwaka 2007. Ilifuatiwa na mwaka mzuri kwa Suarez.

Jans: "Ukifanya vyema kwenye Groningen unavutia vilabu vingine na Ajax ilikuja. Haikuwa hali nzuri na alitaka kwenda, alitaka kuondoka.

"Ndoto yake ilieleweka, nilizungumza naye, lakini klabu pia ilikuwa kwenye mazungunzo na Ajax na ilichukua wiki chache na kulikuwa na changamoto.

"Nimefurahishwa jinsi alijifunza kwa haraka uwanjani, chumba cha kubadilisha, kwenye timu na pia binafsi kama mtu. Taaluma yote ya Suarez na mabadiliko- kutoka Uruguay, kwenda Groningen, kwenda Ajax , kwenda Liverpool hadi Barcelona.

Pande mbili za Suarez

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez alikutana na mke wake Sofia akiwa na miaka 15, na kumfuata hadi Ulaya

Suarez amekuwa akifunga mabao siku za awali huko uholanzi, lakini mbinu anazotumia mshamuliaji huyo pia zimekuwa zikimtia matatani na wakosoaji na pia marefa,

Jans: Kila analotaka ni kushinda kwa vyoyote vile. Nchini Uholanzi na Uingereza ni kitu sawa, hatupendi wakati unapiga mbizi au kuomba kupewa kadi ya njano.

"Nje ya uwanja yuko sawa kabisa, hana kiburi. Anapenda kufanya mzaha. Ni mtu wa familia. Mpenzi wake wa kwanza ndiye mke wake, yuko sawa na familia yake na watoto wake sasa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez amepigwa marufuku mara tatu kwa kuwang'ata wachezaji

Akiwa Ajax ndiko alipigwa marufuku mara tatu kwa kuwang'ata wachezaji-marufuku ya mechi saba kufuatia kisa na mchezaji wa PSV Eindhoven's Otman Bakkal.

De Boer: "Kilikuwa kitu kigumu kwa kila mtu. Unajaribu kumsaidia ajiepushe na vitu kama hivyo lakini ni kitu kilicho ndani yake. Kwa sasa amekomaa zaidi. Lakini kwa kila mtu hasa kwake mwenyewe kilikuwa kipindi kigumu.

Kuondoka Ajax

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez alitajwa mchezaji wa mwaka msimu wake wa mwisho huko Ajax

Katika kipindi cha miaka mitatu unusu huko Amsterdam, Suarez alifunga mabao 111 kwenye mechi 159. Ilichochea liverpool kulipa pauni milioni 22.7 kwa mshambuliaji huyo kuelekea Anfield Januari mwaka 2011.