Nyota ya Ronaldo yazidi kung'aa huku ile ya Messi ikififia

Ronaldo akifunga penalti Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ronaldo akifunga penalti

Ronaldo aliweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao kwenye mashindano 8 mfululizo.

Pia alifunga hetriki yake ya 51 kwa klabu na taifa. Kweli umekuwa ni usiku wa Cristiano Ronaldo.

"Ukiwa unacheza dhidi ya staa kama Ronaldo, mambo haya hutarajiwa," alisema kocha wa Uhispania Fernando Hierro.

"Cristiano ni mchezaji bora duniani na natumai atadumisha fomu yake Qatar na kufunga bao," alisema kocha wake Fernando Santos, ambaye anahisi kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 anaweza kuendelea kuichezea Ureno hadi 2022.

Mechi hiyo ni mojawapo ya mechi bora nilizoshuhudia katika kombe la dunia haswa hatua ya makundi

Lakini licha ya yote, ubora wake unaweza kufafanuliwa namna gani?

Nyota huyu wa Ureno alimiminiwa sifa kufuatia mchezo wake kwenye mchuano utakaokumbukwa kwa kipindi kirefu.

Ronaldo, anavyofahamika, alibadili mkondo wa mchuano kati yao na Uhispania.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Messi akawaza na kuwazua baada ya kukamilika kwa mechi dhidi ya Iceland

Licha ya kuwa na wiki yenye sarakasi ikiwemo kumuachisha kazi kocha wao siku moja tu kabla ya kombe, Uhispania walisalia na dakika chache kujinyakulia ushindi.

"Sihisi nitashuhudia mchuano wa aina hiyo tena. Nitajikatia tiketi nirejee Uingereza," alitania winga wa zamani wa Uingereza Chris Waddle.

Kwani Ronaldo alifanyaje?

Ilimchukua dakika tatu tu nahodha huyo wa Ureno kujitambulisha kwenye mechi kule Sochi. Alitia kimiani bao lake kufuatia penalti waliotunukiwa baada ya kuangushwa na Nacho.

Diego Costa aliisawazishia Uhispania baadaye kidogo lakini kwa mara nyingine, Ronaldo akaiweka Ureno kifua mbele kufuatia kosa la David de Gea.

Mchuano ulirejea sare ya 2-2 baada ya Costa kuifungia Uhispania. Ushindi ulionekea kuegemea wekundu wa Uhispania na mchuano ukawa 3-2 baada ya kunyakua uongozi muda mchache baadaye kupitia bao nzuri la Nacho.

Muda wa Mkwaju wa ikabu wa Ureno ukawasili...

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ronaldo baada ya kufunga hatrick

Ronaldo alijipa bao lake la tatu kupitia mkwaju wa Ureno. Hakuna aliyetia shaka juu ya ni nani angeupiga mkwaju huo. Ronaldo alisonga karibu na mpira huku De gea akiandaa ukuta wa uhispania.

La kushangaza ni kuwa, staa huyo alikuwa akisubiri goli lake kupitia mkwaju wa ikabu baada ya majaribio 45 katika mashindano makubwa.

"Kuna baadhi ya watakaoniuliza kwa nini kipindi cha kwanza nilieleza Ronaldo alihitaji kujiimarisha katika upigaji mkwaju. Ni kwa sababu alijaribu mara 45 na hatimaye alifaulu," alifunguka Nahodha wa zamani wa Uingereza Alan Shearer.

"Ni shuti nzuri na kwa hakika sio rahisi," aliongeza kiungo wa zamani wa Uingereza Danny Murphy.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho alichangia mjadala huo.

Akizungumza na shirika la habari la Urusi, Russia Today, Mourinho alisema fomu ya Ronaldo ya upigaji mkwaju ulififia tangu siku zake Old Trafford na hapo mwanzoni alipojiunga na Real Madrid.

"Kuna wachezaji wa baadhi ya mechi, kuna wale wa kila mechi, na wachezaji wa mechi maalum. Wachezaji wa mechi spesheli nidio walio na umuhimu," alimaliza Mreno huyo.

Sawa na Puskas - Kwa takwimu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Messi baada ya kupoteza Penalti dhidi ya Iceland

Baada ya kufunga mabao yake ya 82, 83 na 84 ya timu ya taifa, Ronaldo amefikia rekodi ya shujaa wa Hungary Ferenc Puskas. Ronaldo anatanguliwa tu na rekodi ya nyota wa Iran Ali Daei mwenye mabao 109.

Baada ya kipenga cha mwisho, licha ya kusifiwa kutokana na fomu yake, Ronaldo alionekana kuangazia ufanisi huo kama wa timu na sio wa kipekee.

"Muhimu ni kuzungumzia juhudi za timu," alisema Ronaldo." Tulisawazisha mchuano ukiwa karibu kumalizika na kwa hivyo tunafuraha.

"Hatujapendekezwa kushinda kombe hili ila tutajitahidi kufanya vyema. Timu inafanya vizuri Zaidi na tutafanya vyema Zaidi."

Mechi za kundi B zitaendelea siku ya Jumatano wiki ijayo Ureno ikipambana na Morocco nayo Uhispania ikichuana na Iran.